• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 25, 2018

  AS VITA YAIFUMUA 4-0 AL MASRY NA KUTINGA FAINALI SHIRIKISHO

  TIMU ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Al Masry ya Misri jana Uwanja wa Martyrs de la Pentecote mjini Kinshasa.
  Kwa matokeo hayo, Vita inaingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 baada ya awali kulazimisha sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Misri na itakutana na Raja Casablanca ya Morocco iliyotioa Enyimba ya Nigeria.
  Mabao ya AS Vita jana yalifungwa na Emomo Eddy Ngoyi mawili dakika ya sita na 39, Jean-Marc Makusu Mundele dakika ya 75 na Mukoko Batezadio dakika ya 90 na ushei.

  Wanaume wa shoka, AS Vita wameingia fainali Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga 4-0 Al Masry ya Misri 

  Mechi nyingine ya marudiano ya Nusu Fainali, Raja Casablanca iliichapa 2-1 Enyimba Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza.
  Mabao ya Raja jana yalifungwa na Zakaria Hadraf dakika ya 45 na ushei na Isiaka Oladuntoye aliyejifunga dakika ya 88, wakati la Enyimba lilifungwa na Abdulrahman Bashir dakika ya 89. 
  Fainali ya kwanza itachezwa Novemba 23 nchini Morocco kabla ya timu hizo kurudiana Novemba 30 mjini Kinshasa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AS VITA YAIFUMUA 4-0 AL MASRY NA KUTINGA FAINALI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top