• HABARI MPYA

    Saturday, July 04, 2015

    PAOLO GUERRERO ATISHA COPA AMERICA, APIGA ZOTE MBILI PERU IKISHINDA 2-0 NA KUMALIZA YA TATU

    MSHAMBULIAJI Paolo Guerrero amefunga bao lake la nne usiku wa kuamkia leo katika Copa America, timu yake ya taifa, Peru ikiifunga Paraguay mabao 2-0 na kushika nafasi ya tatu kwa mara ya pili mfululizo kwenye mashindano hayo.
    Guerrero aliifungia dakika ya 89 kukamilisha ushindi wa Peru.
    Pia aliseti bao la kwanza la timu yake dakika ya 48 akimiliki vizuri mpira wa kona pili uliopigwa na Christian Cueva kabla ya kumpasoa kiungo Andre Carrillo aliyefunga.
    Guerrero sasa amefunga jumla ya mabao saba katika mechi 10 zilizopita za Peru kwenye Copa America.
    Alipiga hat-trick dhidi ya Bolivia kwenye Robo Fainali na akafanya hivyo pia dhidi ya Venezuela katika mechi ya mwisho ya Peru Copa ya mwaka 2011, wakati Peru pia ilipomaliza kwenye nafasi ya tatu.
    Bao lake la jana linamfanya sasa alingane kwa mabao na Eduardo Vargas wa Chile katika michuano ya mwaka huu.
    wenyeji Chile leo wanaikaribisha Argentina katika fainali leo, wakisaka taji la kwanza katika miaka 99 ya historia yamichuano hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAOLO GUERRERO ATISHA COPA AMERICA, APIGA ZOTE MBILI PERU IKISHINDA 2-0 NA KUMALIZA YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top