• HABARI MPYA

    Saturday, July 04, 2015

    FALCAO KULIPWA NUSU MSHAHARA CHELSEA KUTOKA ULE WA MAN UNITED

    MSHAMBULIAJI Radamel Falcao amekubali punguzo la asilimia 50 ya mshahara ili kuthibitisha hajachemsha katika Ligi Kuu ya England.
    Uhamisho wa mkopo wa muda mrefu wa msimu wa Mcolombia huyo ulikamilika jana, hivyo nafasi nyingine mshambuliaji huyo kuonyesha makali yake England baada ya kufeli msimu uliopita akiwa na Manchester United.
    Mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye ana Mkataba na Monaco, mshahara wake ulikuwa ni Pauni 285,000 kwa wiki Old Trafford, lakini umeshuka hadi Pauni 140,000 Stamford Bridge.
    Chelsea imemsajili mshambuliaji wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Monaco

    UHAMISHO WA MKOPO WA PAUNI MILIONI 25 WA FALCAO ULIVYOBUMA MAN UTD

    Ada ya mkopo waliyolipwa Monaco: Pauni Milioni 6
    Mshahara: Pauni 285,000 kwa wiki + posho mbalimbali
    Mechi alizocheza Ligi Kuu: 26
    Mabao aliyofunga Ligi Kuu: 4 
    "Nina furaha sana kujiunga na Chelsea na nina shauku ya kuanza mazoezi na kuisaidia timu dhamira ya kutetea ubingwa wa ligi na kupata nafanikio Ulaya," amesema Falcao.
    Chelsea ina fursa ya kumnunua moja kwa moja Falcao msimu ujao kama atafufua makali yake yaliyomfanya awe miongoni mwa washambuliaji wa kuogopwa Ulaya.
    Louis van Gaal alipomsajili mshambuliaji huyo ilionekana kama amelamba dume msimu uliopita Old Trafford, lakini bahati mbaya mambo hayakuwa kama yalivyotarajiwa. Falcao alimaliza msimu akifunga mabao manne tu katika mechi 29 alizoichezea United na kocha Van Gaal akaghairi mpango wa kumsajili 'jumla'.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCAO KULIPWA NUSU MSHAHARA CHELSEA KUTOKA ULE WA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top