ENGLAND imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia wanawake nchini Canada kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani leo.
Dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na katika dakika 30 za nyongeza, ndipo England wakajibebea Medali ya Shaba/
Ilikuwa ni dakika ya 108 wakati refa Ri Hyang-ok alipowapa penalti England baada ya beki wa Ujerumani, Tabea Kemme kumuangusha Lianne Sanderson kwenye eneo la hatari.
Fara Williams, ambaye alifanya vizuri katika mikwaju ya penalti kwenye mechi dhidi ya Colombia na Japan, akamchambua vizuri kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer na kuamsha bonge la shangwe kwa Waingereza wote waliokuwapo uwanjani.
Fara Williams akishangilia baada ya kuifungia England bao pekee dhidi ya Ujerumani PICHA ZAIDI GONGA HAPA



.png)
0 comments:
Post a Comment