• HABARI MPYA

    Sunday, July 05, 2015

    CHILE MABINGWA COPA AMERICA 2015, ARGENTNA YAPIGWA 4-1 SANTIAGO

    Sanchez akiwa ameinua Kombe akishangilia na wenzake usiku huu
    MCHEZA kwao hutuzwa, naam. Usemi huo umedhihirika usiku huu baada ya wenyeji Chile kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Amerika Kusini, maarufu kama Copa America kwa ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Argentina Uwanja wa Taifa mjini Santiago.
    Baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 120, mshambuliaji wa Arsenal ya England, Alexis Sanchez alifunga penalti ya nne ya Chile na kumaliza mchezo, baada ya Gonzalo Higuain na Ever Banega kukosa mfululizo mikwaj yao. 
    Waliofunga penalti za Chile mbali na Sanchez wengine ni Charles Aranguiz, Arturo Vidal na Matias Fernandez, wakati Lionel Messi alifunga penalti pekee ya Argentina. Scorer of the winning penalty Sanchez whips off his shirt as he celebrates Chile's historic Copa America victory
    Mfungaji wa penalti ya ushindi, Sanchez akiwa amevua jezi yake kukimbia kushangilia  PICHA ZAIDI GOGA HAPA

    Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on FacebookKiungo wa Argentina, Angel di Maria alilazimika kutoka nje kipindi cha kwanza baada ya kuumia nyama.
    Hii inakuwa fainali ya pili mfululizo ya michuano mikubwa Argentina inapoteza, baada ya awali kufungwa na Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia katikati ya mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHILE MABINGWA COPA AMERICA 2015, ARGENTNA YAPIGWA 4-1 SANTIAGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top