Na Philipo Chimi, SHINYANGA
MECHI ya mwendelezo baina ya wenyeji Stand United na Mtibwa Sugar ya Morogoro iliyochezwa asubuhi ya leo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga imemalizika bila ya timu hizo kufungana.
Maana yake, Stand United inanufaika na bao lililofungwa na Haroun Chanongo (pichani) dakika ya 14 jana jioni kabla ya mechi hiyo kuvunjika dakika ya 34 kutokana na mvua kubwa kunyesha na kuharibu mandhari ya Uwanja, hivyo kushinda 1-0.
Matokeo hayo yanaifanya Stand United ifikishe pointi 24, baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya nane kutoka ya 13, ikiishushia nafasi ya tisa Mtibwa Sugar inayobaki na pointi zake 23.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliokuwa ufanyike juzi baina ya Kagera Sugar na Simba SC lakini ukaahirishwa kwa sababu ya mvua pia, utachezwa jioni ya leo.
Kikosi cha Stand United kilikuwa; Mohamed Makaka, Revocatus Richard, Abuu Ubwa, Peter Mutabuzi, Jisend Maganga, Reyna Mgungila, Pastory Athanas, Haruna Chanongo/Yassin Mustafa, Abasalim Chidiebele, Heri Mohamed/Chinedu Mkwene na Vitalis Mayanga/John Ngaga.
Mtibwa Sugar; Saidi Mohammed, Said Mkopi, Majaliwa Mbaga, Andrew Chikopi, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Mgosi, Muzamil Selemba, Ame Ally, Mohamed Ibrahim, Vincent Baranabas na Mohamed Mkopi.

.png)
0 comments:
Post a Comment