KOCHA Arsene Wenger anashawishika kusema hatimaye mambo yanakuwa mambo Arsenal tena - na kila mmoja anaweza kuisikia harufu hiyo.
The Gunners iliirarua 4-1 Liverpool Uwanja wa Emirates Jumamosi mchana, ambao ulikuwa ni ushindi wa saba mfululizo kwao katika Ligi Kuu ya England, ambao unawapandisha hadi nafasi ya pili.
Wakati Manchester City inaweza kurudi nafasi ya pili iwapo itaifunga Crystal Palace leo, nyuma ya vinara Chelsea wanaaoongoza kwa pointi saba, hakuna shaka Wenger akiwa ana kikosi chake kamili ataendelea kupambana.
Mesut Ozil akipongezwa na wenzake baada ya kufunga Jumamosi dhidi ya Liverpool
Hata hivyo, mafanikio haya yanakuja kwa Wenger baada ya kupitia msimu mgumu akitolewa kwenye michuano ya Ulaya na Monaco, na sasa nvuvu zote zipo kwenye kumaliza vizuri na kutetea Kombe la FA.
"Tuko vizuri kwa sasa na tumeimarika kama timu. Kuna vitu vinatokea, ambavyo vinakuonyesha wewe kwamba wapo tayari kupambana kila mmoja,". Wenger amepanoa kuifunga Chelsea Uwanja wa Emirates Aprili 26 ili kupunguza pengo la pointi.


.png)
0 comments:
Post a Comment