• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 18, 2020

  TFF YAUNDA KAMATI MPYA YA WAAMUZI MWENYEKITI SOUD ABDI, MAKAMU WAKE NKONGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyokutana leo imefanya mabadiliko katika Kamati ya waamuzi na kuunda kamati mpya.
  Hiyo ni kufuatia kikao cha pamoja baina ya Kamati ya Waamuzi iliyovunjwa chini ya Mwenyekiti, Salum Chama na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na Kamati ya Mashindano ya TFF kujadili matatizo ya waamuzi nchini.
  Na kikao hicho kilifuatia agizo la Rais wa TFF, Wallace Karia kufuatia malalamiko mfululizo juu ya uchezeshaji mbovu wa waamuzi katika Ligi Kuu.

  Kamati mpya iliyotajwa leo inaundwa na watu watano chini ya Mwenyekiti, Soud Abdi na Makamu wake, Israel Nkongo na Wajumbe Zahra Mohammed, John Kanyenye na Samuel Mpenzu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAUNDA KAMATI MPYA YA WAAMUZI MWENYEKITI SOUD ABDI, MAKAMU WAKE NKONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top