• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 26, 2020

  LUC EYMAEL NA TSHISHIMBI WAPIGWA FAINI KWA KUGOMA KUZUNGUMZA NA AZAM TV TANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga SC, Mbelgiji Luc Eymael ametozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na mdhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Azam Media Februari 23, mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
  Eymael alifanya kosa hilo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na adhabu imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 41(2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
  Kosa kama hilo lilifanuywa pia na Nahodha wa Yanga SC, Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye yeye ametozwa faini ya Sh. 200,000.
  Tshishimbi naye alikataa kufanya mahojiano na Azam TV baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0 Uwanja wa Mkwakwani na adhabu yake imetolewa kwa mujibu wa kanuni 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUC EYMAEL NA TSHISHIMBI WAPIGWA FAINI KWA KUGOMA KUZUNGUMZA NA AZAM TV TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top