• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 15, 2020

  UEFA YAIFUNGIA MANCHESTER CITY MIAKA MIWILI LIGI YA MABINGWA

  KLABU ya Manchester City jana ilifungiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa misimu miwili ijayo.
  Mabingwa hao wa England wamechukuliwa hatua hiyo baada ya kuvunja kanuni ya matumizi ya fedha kiungwana katika usajili ambayo imewekwa na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).
  Manchester City wanashutumiwa kufanya makosa hayo kati ya mwaka 2012 na 2016 na pamoja na kufungiwa, pia wamepigwa faini ya Pauni Milioni 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UEFA YAIFUNGIA MANCHESTER CITY MIAKA MIWILI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top