• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 15, 2020

  POLISI TANZANIA YAIBUKA NA USHINDI WA MABAO 3-2 DHIDI YA WENYEJI, KMC UWANJA WA UHURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  TIMU ya Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Polisi kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro, yamefungwa na Marcel Kaheza dakika ya 10, Matheo Anthony (pichani kushoto) dakika ya 39 na Baraka Majogoro dakika ya 87, wakati ya KMC yamefungwa na Abdul Hillary dakika ya 80 na Ally Ramadhani dakika ya 83.
  Polisi inafikisha pointi 33 baada ya ushindi wa leo kwenye mchezo wa 22 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba, ikiishusha JKT Tanzania, wakati KMC inabaki nafas ya 15 kwenye ligi ya timu 20 kwa pointi zake 21 za mechi 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAIBUKA NA USHINDI WA MABAO 3-2 DHIDI YA WENYEJI, KMC UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top