• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 21, 2020

  MASHINDANO YA KUOGELEA YA TALISS-IST KUFANYIKA JUMAMOSI NA JUMAPILI BWAWA LA MASAKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  KLABU mbalimbali za mikoani zimewasili jijini Dar es Salaam tayari kupambana katika mashindano maarufu ya kuogelea ya Taliss-IST yaliyopangwa kufanyika Jumamosi na Jumapili kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST-Masaki).
  Waogeleaji kutoka Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar na Morogoro wamekwisha wasili tayari kwa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Jubilee Insurance, Nissan na Azam. Jumla ya waogeleaji 249 watashiriki katika mashindano hayo.
  Meneja wa klabu ya Taliss-IST ambaye pia ni mratibu wa mashindano hayo, Hadija Shebe alisema kuwa wanatarajia kuona ushindani mkali kutoka kwa waogeaji hao wa mikoani na wa Dar es Salaam.
  Wakati Mwanza itawakilishwa na MSC, Morogoro itawakilishwa na Mis Piranhas huku Arusha itawakilishwa na Braeburn. Pia katika mashindano hayo kutakuwa na klabu ya UWCEA ambayo inaundwa na waogeleaji wa Moshi na Arusha.


  Nyota wa kuogelea, Franco Du Plessis akionyesha uwezo wake katika mashindano ya kuogelea

  Dar es Salaam itawakilishwa na klabu maarufu kama Dar es Salaam Swimming Club (DSC), Bluefins na wenyeji wa mashindano hayo, Taliss-IST. Zanzibar itawakilishwa na ISZ maarufu kwa jina la Wahoo.
  Alisema kuwa jumla ya staili tano zitashindaniwa na waogeleaji katika mashindano hayo. Staili hizo ni free, butterfly, backstroke, breaststroke na Individual Medley.
  Waogeleaji watashindana katika umri tofauti ambao ni chini ya miaka nane, miaka tisa na 10, miaka 11 na 12, 13 na 14 na kuanzia miaka 15 na kuendelea. Alisema pia kutakuwa na mashindano ya wazi ambayo yatashirikisha waogeaji wenye umri tofauti.
  "Kutakuwa na jumla ya mashindano 105 ambapo siku ya kwanza, waogeleaji watashindana katika mashindano 71 na siku ya pili watamzalizia. Washindi katika kila umri watazawadiwa vikombe na washindi katika kila tukio watazawadiwa medali mbalimbali,” alisema Hadija.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHINDANO YA KUOGELEA YA TALISS-IST KUFANYIKA JUMAMOSI NA JUMAPILI BWAWA LA MASAKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top