• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 14, 2020

  TANZANIA PRISONS YAPEWA ‘USHINDI WA MEZANI’ DHIDI YA RUVU SHOOTING MLANDIZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  TIMU ya Tanzania Prisons FC imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu dhidi ya Ruvu Shooting FC kwenye mchezo uliokuwa ufanyike Februari 11, 2020 mwaka huu Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani.
  Mchezo haukufanyika baada ya mwenyeji, Ruvu Shooting kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance) uwanjani kama Kanuni ya 14 (2l) inavyosema na kusababisha mchezo kuvunjwa na mwamuzi baada ya kusubiri kwa dakika 30 bila gari hiyo kutokea. 
  Naye mchezaji wa Mwadui FC, Hashim Yahya Mussa amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kuwaonyeshea kidole cha kati watazamaji kama ishara ya matusi baada ya filimbi ya kumaliza mchezo ilipopigwa.
  Mchezaji huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho katika mchezo uliofanyika Februari 8, mwaka huu Uwanja wa Namfua mjini Singida.
  Nayo klabu ya Yanga SC imepewa Onyo kali kwa kosa la kuwakilishwa na watu pungufu ya idadi inayotakiwa katika kikao cha maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na kujaza jina la Kocha wa walinda milango Peter Manyika kuwa amehudhuria kikao hicho wakati hajahudhuria.
  Kitendo hicho kilifanyika katika maandalizi ya mchezo uliofanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
  Katika daraja la Kwanza; Meneja wa timu ya Gipco, Ayubu Msonge amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga teke mwamuzi wa mchezo namba 80 wakifungwa 2-1 na Gwambina. 
  Alifanya hivyo FC baada ya mchezo kumalizika pindi waamuzi walipokuwa wanatoka uwanjani, kitendo hicho kilifanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.
  Nayo Gipco imetozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kutokana na timu hiyo kushindwa kuhakikisha usalama kwenye mchezo uliofanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Nyankumbu ikiwa ni jukumu lao kama timu mwenyeji, hivyo kutokea vurugu zilizosababisha kupigwa kwa afisa wa Bodi ya Ligi na waamuzi wa mchezo huo tajwa katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.
  Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43 (1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Uthibiti wa Klabu.
  Kamati imeieleza timu ya Gipco FC kuwa endapo vitendo hivyo vitajirudia tena katika mchezo mwingine watakaocheza, haitasita kuchukua maamuzi makubwa zaidi ikiwemo kuwabadilishia uwanja wa nyumbani wa klabu yako (home ground) na kupangiwa uwanja mwingine.

  Mechi namba 78- Transit Camp FC 4 vs Mawenzi FC 0-- Meneja wa timu ya Mawenzi Fc Christopher Mapunda amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kutoa lugha za matusi katika mchezo huo tajwa uliofanyika February 2, 2020 katika uwanja wa Uhuru jjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAPEWA ‘USHINDI WA MEZANI’ DHIDI YA RUVU SHOOTING MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top