• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 09, 2020

  NCHI ZA KASKAZINI ZILIVYOFANIKIWA ZAIDI KUITAWALA SOKA YA AFRIKA

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  NCHI za Kaskazini, Kusini na Magharibi mwa Afrika zimepiga hatua kiasi kwenye maendeleo ya soka kiasi cha vilabu na wachezaji wao kuwa sehemu ya mpira wa wa Dunia kwa maana ya kwamba wanafahamika na kuzungumzwa kila kona ya ya Dunia ya wapenda soka mfano mzuri Sadio Mane na Mohamed Salah.
  Lakini pamoja na maendeleo hayo,tutazame zaidi ukanda wa Afrika ya Kaskazini ambayo kwa kiasi kikubwa imetawaliwa na nchi za kiarabu kama  Misri,Algeria,Morocco, Tunisia na nyinginezo,jamaa wapo siriasi na mpira sana,hawana mzaha linapokuja suala la kuweka pesa kwenye mpira,mfano mzuri unaweza kuitazama Pyramids FC, hii ni timu ngeni kabisa lakini wamewekeza paundi milioni 500,jaribu kuongeza volume uwafikirishe na wenzio,mafanikio yao hayaji tu.
  Majuzi tu ratiba ya robo fainali Afrika (klabu bingwa na shirikisho) imetoka na ukanda huu wa Afrika kaskazini wametoa kwa ujumla timu 11 kati ya 16 zinazopaswa kucheza Robo fainali ya klabu bingwa na shirikisho,unaweza kuwapa asilimia kubwa ya kutwaa ubingwa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya timu zilizofika hatua hiyo,siku zote namba huwa hazidanganyi.
  Ukiangalia kwa makini utagundua si vilabu vyao tu,bali hata timu zao za taifa zinafanya poa sana,mara kwa mara zinashiriki mashindano makubwa kama kombe la Dunia,kombe la mataifa ya Afrika na hata mashindano ya Olimpiki,wanajali sana sokala vijana,na huko ndipo wanapomwaga pesa za kutosha,wanasomesha makocha wao ili kujakutunza vipaji vikubwa walivyonavyo.
  Siri kubwa iliyojificha kuwa ni kwa nini wachezaji wanaotoka Kaskazini mwa Afrika wanaocheza kwenye Ligi kubwa duniani ni wachache mno kuliko wanaotoka Magharibi mwa Afrika, sababu kubwa ni kwamba timu za kaskazini mwa Afrika zinalipa mishahara mikubwa mno na hata baadhi ya wachezaji wa Magharibi mwa Afrika wamezamia hapo Kaskazini, hawataki kutoka japo wana uwezo wa kucheza Ulaya. Ndiyo maana mchezaji anatoka Stoke City anakuja kucheza Al Ahly kwa mkopo, si jambo rahisi kabisa.
  Bado naiona Afrika Kaskazini wakilitawala sana soka la Afrika kutokana  na namna ambavyo wapo siriasi,kama hujapanda huwezi kuvuna, usitarajie kupata kwenye hakuna.

  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti zake za instagram na Twitter: Twitter: @dominicksalamb1   Instagram: @dominicksalamba au namba +255 713 942 770)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NCHI ZA KASKAZINI ZILIVYOFANIKIWA ZAIDI KUITAWALA SOKA YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top