• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 25, 2020

  MANE APIGA BAO LA USHINDI JIONI LIVERPOOL YAICHAPA WEST HAM 3-2

  Sadio Mane akitabasamu baada ya kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya 81 ikiichapa 3-2 West Ham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Anfield, Liverpool. Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya tisa na Mohamed Salah dakika ya 68, wakati ya West Ham United yalifungwa na Issa Diop dakika ya 12 na Pablo Fornals dakika ya 54 na kwa ushindi huo kikosi cha Jurgen Klopp kinafikisha pointi 79 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 22 zaidi ya Manchester City inayofuatia nafasi ya pili 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANE APIGA BAO LA USHINDI JIONI LIVERPOOL YAICHAPA WEST HAM 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top