• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 22, 2020

  YANGA SC YATOZWA FAINI, MORRISON APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU KWA KUMPIGA MCHEZAJI WA PRISONS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga SC imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la timu hiyo kushindwa kuwasilisha fomu ya wachezaji wao kwenye kikao cha kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 0-0 Februari 15, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almasi Jumapili Kasongo kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Hatua hiyo imefuatia kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichofanyika jana kupitia taarifa mbalimbali za mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili (SDL) zinazoendelea hivi sasa nchini.
  Aidha, kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Mghana Bernard Morrison amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons, Jeremia Juma wakati mpira ukiwa umesimama siku hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YATOZWA FAINI, MORRISON APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU KWA KUMPIGA MCHEZAJI WA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top