• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 22, 2020

  NAMUNGO FC YAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUJIWEKA SAWA KWENYE NAFASI YA TATU LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, RUANGWA
  TIMU ya Namungo FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Matokeo hayo yanaifanya Namungo FC ijiweke sawa nafas ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikifikisha pointi 43 katika mchezo wa 23, sasa ikizidiwa pointi mbili tu na Azam FC walio nafasi ya pili ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.
  Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na Nassor Mwinchui, aliyesaidiwa na Khalfan Sika wote wa Pwani na Rashid Zongo wa Irnga, bao pekee la Namungo FC limefungwa na mshambuliaji na Nahodha wake, Reliants Lusajo dakika ya 60.


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imeichapa 3-1 Ruvu Shooting mabao yake yakifungwa na Marcel Kaheza mawili dakika ya 13 na 23 na Jimmy Shoji dakika ya 27, huku la wageni likifungwa na kiungo mkongwe, Shaaban Kisiga ‘Malone Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Na bao pekee la Peter Mapunda kwa penalti dakika ya 28 likaipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjin Mbeya.
  JKT Tanzania nayo ikaichapa Kagera Sugar 1-0, bao pekee la Hassan Materema dakika ya 41 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 
  Ndanda FC ikaichapa KMC 2-1 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, mabao yake yakifungwa na Kiggi Makasi dakika ya pili na Abdulrazack Ramadhan dakika ya 70, huku Mohamed Samatta akiwafungia wageni dakika ya 77.
  Mbao FC imepoteza mechi nyumbani baada ya kuchapwa 2-1 na Mwadui FC.  Mabao ya Mwadui yamefungwa na Jackson Shiga dakika ya 65 na Raphael Aloba dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Mbao FC limefungwa na Wazir Junior dakika ya 80.
  Kikosi cha Namungo FC kilikuwa; Nourdine Balora, Miza Chrstom, Jukumu Kibanda, Carlos Protas, Stephen Duah, Daniel Joram, Hashim Manyanya/George Makang'a dk66, Nzigimasabo Steve, Bigirimana Blaise, Lucas Kikoti na Reliants Lusajo.
  Azam FC; Razack Abalora, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohamed, Bryson Raphael, Joseph Mahundi, Abdallah Masoud/Shaaban Chilunda dk75, Andrew Simchimba/Richard Djodi dk60, Obrey Chirwa/Donald Ngoma dk76 na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUJIWEKA SAWA KWENYE NAFASI YA TATU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top