• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 26, 2020

  MAREFA WALIOKATAA BAO LA POLISI DHIDI YA YANGA MOSHI WAFUNGIWA MIEZI MITATU KILA MMOJA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAREFA waliochezesha mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya wenyeji, Polisi Tanzania na Yanga SC ya Dar es Salaam Abel William na Martin Mwalyaje wamefungiwa miezi mitatu kila mmoja kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mchezo huo Februari 18, mwaka huu Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Polisi Tanzania walilazimishwa sare ya 1-1 na Yanga SC, lakini marefa hao walikataa bao moja zuri la wenyeji lililofungwa na mshambuliaji Matheo Anthony (pichani).
  Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imesema kwamba William na Mwalyaje wamefungiwa kwa mujibu wa kanuni ya 39 (1A) ya Udhibiti wa Waamuzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WALIOKATAA BAO LA POLISI DHIDI YA YANGA MOSHI WAFUNGIWA MIEZI MITATU KILA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top