• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 11, 2020

  KITU WANACHOTAKA MASHABIKI WA SOKA NI USHINDI TU KWA TIMU ZAO

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  Umeshawahi kuona mtu akiwa kwenye sherehe za kufunga ndoa?
  Kama hujawahi kuona ngoja nikusimulie kidogo,huwa ni wakati mzuri si kwa bwana harusi au bibi harusi pekee bali kila mtu ushangilia kwa nderemo na vifijo utawala kifupi huwa ni shangwe.👏🏽👏🏽
  Inakuwa ni vigumu kujua nani anafuraha ya kweli au anaigiza,ila baada ya ndoa kupita kinachofuata ni maisha ya Bwana na Bibi harusi raha zitakuwa zao pia na shida hubakia kuwa zao na ikizidi kufikia kuachana basi jamii ile iliyoshangilia sherehe za ndoa uwageuka na kuwaona wa ajabu kwa kadri ya utashi wa wanajamii.
  Rudi hapa iwe kocha au mchezaji anaposajiliwa mambo huwa ni moto ni mwendo wa sifa zilizopitiliza ila ukiendelea zaidi ndiyo utajua nini maana ya mashabiki.
  Hawa mashabiki si wengine ni wale mashabiki wa soka,kandanda,kabumbu  na majina mengine mengi lukuki.
  Ndio mana leo nimeamua kuja na mashabiki na mchezo wa soka ili twende sawa. Soka ndio mchezo unaopendwa zaidi,namaanisha una mashabiki wengi zaidi,kwa nini unapendwa sana?
  inawezekana ni kutokana na jinsi unavyochezwa,namna ulivyo na ushindani,lakini pia hukutanisha hisia za watu wengi zaidi.
  Mashabiki hao wa soka wala hawahitaji taaluma yoyote ili kufuzu kupewa cheo hicho cha ushabiki,ni mapenzi tu ambayo mwisho wa siku hukutanisha watu wenye hisia mfanano na kujikuta wanakua kundi moja linalosapoti sana timu fulani.
  Hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa sana hasa timu  zinapokosa matokeo ya ushindi,mashabiki hulipuka na kusema timu inacheza hovyo sana,kocha hafai na kuongeza presha kwenye timu jambo ambalo linapoteza muelekeo wa timu husika.
  Kocha yeyote,anapokwenda kwenye timu yeyote,anajua wazi kuwa presha mbaya zaidi itakayohatarisha kibarua chake ni presha ya mashabiki,kwa kulijua hilo kocha anapaswa afanye kazi kwelikweli,hapo ndipo uhakika wa kubaki katika timu utakuwepo.
  Wanachokifanya mashabiki wa kibongo kwa sasa wanakosea? ukidhani hivyo wewe ndio utakua unakosea zaidi,shabiki anataka matokeo ya ushindi tu,anaweza kuelewa timu ikipata sare au hata ikifungwa lakini inaonekana wazi inacheza soka safi,kipimo cha makocha wengi siku hizi kimekuwa ni kuridhika kwa mashabiki,ili kocha aweze kuyaepuke hayo lazima afanye kazi kwa nguvu zote,tofauti na hapo ataondolewa tu.
  Kumwambia shabiki kuwa leo tumefungwa asiongee maana jana tulishinda wakati ni wazi anaona timu inacheza vibaya,,haina mipango,ni kupoteza  muda,haisaidii kitu zaidi ya kumfanya shabiki azidi kuongea hovyo na kuongeza presha kwenye timu,tiba ya kichaa cha shabiki ni soka safi na ushindi tu.
  Huwa nacheka wakati mwingine makocha wanakera mashabiki wa timu wanazofundisha mpaka mashabiki wanajigeuza kuwa makocha,utasikia pale angempanga fulani,unamuona fulani hastahili kabisa kucheza hapa tayari imani ya mashabiki kwa kocha wao huwa imetoweka na kuwa sawa na sifuri.
  Wakati kocha husika akipewa kandarasi mambo huwa safi,pande zote ujinasibu ni mwendo wa sifa za kutukuka na matumaini yaliyozidi kiasi juu ya mwalimu huyo  huku wakijinasibu kuwa wamesajili zaidi ya kocha wa kawaida. 
  Hapa ndipo unikumbusha sherehe zile za harusi kwani zinapokwisha na kila kitu kwa washangiliaji nacho hupotea.
  Hakuna namna ndoa ya kocha na mashabiki inaweza kudumu zaidi ya matokeo mazuri kwa Timu husika kinyume na hapo swala la kuondoka litakuhusu.
  Mashabiki wa soka wanajua matokeo matatu kwa kuyasema ila kwenye vilabu vyao wanatambua na kuishi na matokeo ya aina moja yani Ushindi, ushindi, ushindi. 

  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika akaunti  zake za instagram na Twitter. Twitter:@dominicksalamb1    Instagram:@dominicksalamba au namba +255713942770)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KITU WANACHOTAKA MASHABIKI WA SOKA NI USHINDI TU KWA TIMU ZAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top