• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 28, 2020

  SHIME ANAAMINI TANZANIA ITAICHAPA UGANDA KESHO KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U-17

  Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM 
  KOCHA Mkuu wa timu ya wanawake u-17  ya Tanzania, Bakari Shime amesema kuwa kikosi kimejipanga kufanya vyema katika mechi  dhidi ya Uganda.
  Timu hiyo ya wanawake inashuka dimbani Jumapili uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kuwakaribisha Uganda katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia nchini India, Julai mwaka huu.
  Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Shime amesema kuwa ana amini kuwa maandalizi yapo vizuri na wanahakikisha watafanya vyema katika mechi hiyo ya hapa nyumbani.
  Alisema kuwa wachezaji wote wapo vizuri na kikosi kina morali ya kuibuka na ushindi  katika mechi hiyo.
  “Kwa mujibu wa ripoti ya daktari hakuna majeruhi wachezaji wote wapo fiti na kufikia siku ya mechi kikosi kitahakikisha kinafanya vyema katika mechi hiyo ambayo ni mechi muhimu kwa taifa" alisema 
  Aliongeza kuwa maandalizi yapo vizuri na wamepanga kufanya vyema nyumbani na ugenini japo mechi utakuwa ngumu lakini  atahakikisha  kikosi kinafanya vyema.
  Naye nahodha wa timu hiyo, Irene Elias alisema   kikosi kimejiandaa kufanya vyema katika mchezo huo japo mechi utakuwa ngumu.
  "Nina Imani Mungu yupo upande wetu tutafanya vyema katika mechi hiyo kutokana na maandalizi ambayo tumefanya," alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHIME ANAAMINI TANZANIA ITAICHAPA UGANDA KESHO KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U-17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top