• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 19, 2020

  DAVID RICHARD APIGA HAT TRICK ALLIANCE YAIFUMUA MWADU 4-1, AZAM FC SARE 1-1 NA NDANDA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Alliance FC imeibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-1 dhidi ya jirani zao, Mwadui FC jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. 
  Kwa ushindi huo, Alliance FC inayofundishwa na Freddy Felix Minziro inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 23, ingawa inabaki nafasi ya 13, wakati Mwadui FC hali ni mbaya zaidi, ikibaki na pointi zake 19 katika nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, baada ya kucheza mechi 22.
  Mabao ya Alliance FC leo yamefungwa na David Richard matatu dakika za tano, 18 na 83 na Sameer Vicent dakika ya 80, wakati bao pekee la Mwadui FC limefungwa na Otu Samuel dakika ya 23.

  Uwanja wa Nangwanda Sijaona wenyeji, Ndanda SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC, wakati Tanzania Prisons nayo imetoka sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya. 
  Uwanja wa Nangwanda Vitalis Mayanga alianza kuifungia Ndanda FC dakika ya 10 kabla ya Andrew Simchimba kuisawazishia Azam FC dakika ya 76.
  Sare ya Azam FC ni nafuu kwa Yanga SC ambayo nayo jana ililazimisha sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
  Azam FC inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu pointi zake 45 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Namungo na Yanga SC zenye pointi 40 kila moja. Lakini Namungo imecheza mechi 22 na Yanga 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DAVID RICHARD APIGA HAT TRICK ALLIANCE YAIFUMUA MWADU 4-1, AZAM FC SARE 1-1 NA NDANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top