• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 08, 2020

  AZAM FC YAICHAPA KMC 3-1 NA KUPUNGUZA IDADI YA POINTI WANAZOZIDIWA NA SIMBA KILELENI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya KMC ya Kinondoni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na kocha Mromania, Aristica Cioaba inafikisha pointi 41 sasa baada ya kucheza mechi 20, ingawa inabaki nafas ya pili nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 50 za mech 20 pia.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji wake Muivory Coast, Richard D’jodi dakika ya 25 na Mzambia Obrey Chirwa mawili dakika ya 33 na 43, huku bao pekee la KMC likifungwa na Sadallah Lipangile dakika ya 84.
  Mechi nyngine za Ligi Kuu leo, bao pekee la mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga Ndama ‘Falcao’ dakika ya 39 lilitosha kuipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Nayo Coastal Union imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania mabao ya Mtenje Albano dakika ya 69 na Mudathir Said dakika ya 90 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Bao pekee la Mwinyi Elias dakika ya 20 likatosha kuipa Lipuli FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo, Morogoro. 
  Nayo Mbeya City ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Tanzana Prisons bao pekee la Peter Mapunda kwa penalti dakika ya 13 Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Bao la dakika ya 65 la Sameer Vincent likaisaidia Alliance FC kupata sare ya 1-1 na Mbao FC iliyotangulia kwa bao la Datius Peter dakika ya 55 kwa penalti Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Singida United nayo ikalazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui FC Uwanja wa Liti, SIngida. Mabao ya Singida yalifungwa na Muharami Issa ‘Marcelo’ dakia ya 61 na 90 na ya Mwadui FC yalifungwa na Venance Ludovic dakika ya 24 na Raphael dakika ya 41.
  Ndanda SC ikalazimishwa sare ya 0-0 na Namungo FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Kagera Sugar nao wakalazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA KMC 3-1 NA KUPUNGUZA IDADI YA POINTI WANAZOZIDIWA NA SIMBA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top