• HABARI MPYA

  Saturday, February 22, 2020

  STAND UNITED WAPIGWA FAINI SH 500,000 BAADA YA MASHABIKI WAKE KUWASHAMBULIA KWA GWAMBINA FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Stand United FC imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la mashabiki wake kufanya vurugu kubwa kwa kurusha mawe kwenye benchi la ufundi la Gwambina FC na kuwapiga waamuzi waliosimamia mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1 Februari 1, mwaka huu Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
  Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 43(1) kuhusu Udhibiti wa klabu na endapo vitendo hivyo vitajirudia tena katika mchezo mwingine watakaocheza, Kamati haitasita kuchukua maamuzi makubwa zaidi ikiwemo kuwabadilishia uwanja wa nyumbani klabu ya Stand United (home ground) na kupangiwa uwanja mwingine.
  Timu ya Mlale FC imepewa Onyo kali kwa kosa la kuchelewa kufika kwenye kikao cha kitaalam cha maandalizi ya mchezo dhdi ya Iringa United FC walioshinda 3-0 bila kutoa sababu kwa msimamizi wa mchezo (Kamisaa) kwenye mchezo uliofanyika Februari 15, 2020 uwanja wa Mkwawa mkoani Iringa.
  Timu ya Geita Gold FC imetozwa faini ya Tsh 200,000 kutokana na kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa ukaguzi na wakati wa mapumziko kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC walioshinda 1-0 Februari 15 Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.
  Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 34 ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Aidha, Geita Gold FC imetozwa faini ya Sh 200,000 kutokana na timu hiyo kutotumia mlango uliokuwa umeandaliwa kwa timu wakati wa kuingia uwanjani na badala yake wakatumia mlango wa jukwaa kuu, kwenye mchezo huo.
  Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(14) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Klabu ya Gwambina FC imetozwa faini ya Tsh 500,000/ (laki tano) kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kufanya matukio ya kuwashambulia na kuwapiga mashabiki wa Geita FC mara kadhaa katika mchezo uliofanyika Februari 15, 2020 uwanja wa Gwambina mkoani Mwanza.
  Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STAND UNITED WAPIGWA FAINI SH 500,000 BAADA YA MASHABIKI WAKE KUWASHAMBULIA KWA GWAMBINA FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top