• HABARI MPYA

    Wednesday, February 26, 2020

    RUVU SHOOTING YAPIGWA FAINI SH MILIONI 1, MASAU BWIRE APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Ruvu Shooting FC imetozwa faini ya Sh Milioni 1 kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kusababisha kutokea kwa vurugu kwenye mchezo huo uliofanyika Februari 22, mwaka huu Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
    Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kwa Vyombo vya Habari leo mjini Dar es Salaam imesema kwamba vurugu hizo ziliongozwa na mwalimu wa timu hiyo Salum Mayanga pamoja na wachezaji wake, Shaaban Kisiga, Emmanuel Martin na Rajab Zahir na adhabu imetolewa kwa mujibu wa Kanuni 14(43) ya Ligi Kuu Kuhusu Taratibu za Mchezo.
    Taarifa ya Kamati pia imesema kwamba ilipitia tena shauri hilo Ruvu Shooting kuomba marejeo juu ya maamuzi ya kuwapa Tanzania Prison FC ushindi dhidi ya kutokana na kutofata Kanuni ya 14(2l) ya Ligi Kuu maamuzi kubaki kama yalivyokuwa.
    Naye Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwenye vyombo vya habari na kauli za maudhi kwa viongozi wa timu ya Polisi Tanzania FC katika mchezo uliochezwa Februari 22, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAPIGWA FAINI SH MILIONI 1, MASAU BWIRE APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top