• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 26, 2020

  WILDER AMFUKUZA KOCHA WAKE ALIYERUSHA TAULO ULINGONI

  BONDIA Deontay Wilder atamfukuza kocha wake Mark Breland baada ya kukasirishwa na kitendo chake cha kurusha taulo ulingoni Jumapili katika pambano lake dhidi ya Tyson Fury. 
  Mmarekani, Wilder alivuliwa taji la WBC uzito wa juu baada ya kuchapwa kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba na Fury ukumbi wa MGM Grand Jijini Las Vegas.
  Na hiyo ni baada ya Breland kurusha taulo ulingoni raundi ya saba kufuatia Wilder kuchapwa ngumi mfululizo bila majibu katika pambano ambalo tayari alikwishaangushwa mara mbili.
  Hata hivyo, mbabe wa Alabama, Wilder amesema aliwazuia watu wa kona yake kusalimu amri licha ya kuzidiwa na wamuache aendelee kwa sababu alikuwa ana raundi tano zaidi kuelekea mwisho wa pambano. 

  Wilder na kocha wake mkuu, Jay Deas walizungumza na Waandishi wa Habari baada ya pambano na kusema hawakukubaliana na uamuzi wa kurusha taulo na kwa hilo atabomoa 'benchi lake la ufundi'.   
  Wilder amesema ataanza kushughulikia pambano la marudiano na ataingia na kocha mpya.  
  "Nimesikitishwa na Mark kwa sababu nyepes tu, tulizungumza juu ya hili mara nyingi na si hasira," alisema Wilder.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WILDER AMFUKUZA KOCHA WAKE ALIYERUSHA TAULO ULINGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top