• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 10, 2020

  SADALLAH LIPANGILE AWAPIKU WADADA NA DILUNGA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU ANUARI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa KMC ya Kinondoni, Sadallah Lipangile amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Januari 2020 akiwashinda Nicholas Wadada wa Azam na Hassan Dilunga wa Simba alioingia nao fainali.
  Baada ya kuhamishwa kutoka nafasi ya ulinzi wa kati hadi kuwa mshambuliaji, mchezaji kiraka wa KMC Sadallah Lipangile amefunga jumla ya magoli matano katika mechi tatu.
  Kati ya magoli hayo matano, manne amefunga katika michezo miwili ya mwezi Januari dhidi ya Singida United (05/01/2020) na dhidi ya Mtibwa Sugar (17/01/2020) huku bao la tano akilifunga wikendi iliyopita dhidi ya Azam FC (08/02/2020). 

  Katika orodha ya wafungaji bora kwenye ligi kuu, hadi sasa Sadallah anakamata nafasi ya 12 akiwa sawa na Ayoub Lyanga (Coastal), Bigirimana Blaise (Namungo), Hassan Dilunga (Simba), Innocent Edwin (Biashara), Shaban Hamis (Coastal) na Kelvin Kongwe (Kagera). Haya hapa magoli matatu kati ya matano aliyofunga.
  Aidha, Aristica Cioaba wa Azam FC ameibuka Kocha Bora wa mwezi huo akiwashinda Sven Vandenbroeck wa Simba na Malale Hamsini wa Polisi Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SADALLAH LIPANGILE AWAPIKU WADADA NA DILUNGA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU ANUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top