• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 10, 2020

  LUKAKU ATIA LA NNE INTER YAITANDIKA MILAN 4-2 SERIE A

  Mshambuliaji Mbelgiji, Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia Inter Milan bao la nne dakika ya 90 na ushei ikitoka nyuma na kuichapa AC Milan 4-2 usiku wa jana kwenye mchezo wa Serie A Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan. Mabao mengine ya Inter Milan yalifungwa na Marcelo Brozovic dakika ya 51, Matias Vecino dakika ya 53 na Stefan de Vrij dakika ya 70 baada ya AC Milan kutangulia kwa mabao ya Ante Rebic dakika ya 40 na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 45 na ushei na kwa ushindi huo sasa kikosi cha Antonio Conte kinalingana pointi na Juventus, 54 baada ya kila timu kucheza mechi 23 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUKAKU ATIA LA NNE INTER YAITANDIKA MILAN 4-2 SERIE A Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top