• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 10, 2020

  KOCHA VANDONBROECK AAHDI KUWAPIGA MTIBWA SUGAR KWA VYOVYOTE VILE KESHO MOROGORO

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  KOCHA Mbelgiji wa Simba SC, Sven Ludwig Vandonbroeck amewaahidi ushindi wapenzi wa timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
  Akizungumza mjini Morogoro leo baada ya mazoezi, Vandonbroeck anayesaidiwa na mzalendo, Suleiman Matola, kocha wa makipa Muharami Mohamed ‘Shilton’ na kocha wa Fiziki, Mtunisia, Adel Zrane – amesema kwamba hakuna sababu ya kuwanyima ushindi kesho na watapambana kuhakikisha hilo linatimia.

  “Hakuna sababu, iwe ni hali ya uwanja, mvua, jua au waamuzi wa mchezo kesho haipaswi kuwa sababu. Ni ushindi pekee ndio tunahitaji na tuna kazi ya kuhakikisha tunafanikisha hilo,” amesema Vandenbroeck kuelekea mchezo wa kesho.
  Vandonbroeck alipoteza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu tangu aanze kazi Simba SC ilipochapwa 1-0 na JKT Tanzania Ijumaa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 
  Pamoja na kipigo hicho, Simba inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 50 za mechi 20 sasa, ikiwazidi pointi 12 Azam FC wanaofuatia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA VANDONBROECK AAHDI KUWAPIGA MTIBWA SUGAR KWA VYOVYOTE VILE KESHO MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top