• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 10, 2020

  CIOABA AWAPIKU VANDENBROECK NA MALALE HAMSINI TUZO YA KOCHA BORA LIGI JUU JANUARI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MROMANIA Aristica Cioaba wa Azam FC ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwezi Januari baada ya kuisaidia klabu yake kupanda hadi nafasi ya pili.
  Cioaba anayeinoa Azam FC kwa mara ya pili, ametwaa tuzo hiyo baada ya akiwashinda Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck wa Simba na mzawa, Malale Hamsini wa Polisi Tanzania.
  Kwa upande wake, mshambuliaji wa KMC ya Kinondoni, Sadallah Lipangile amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu mwezi Januari akiwashinda Nicholas Wadada wa Azam na Hassan Dilunga wa Simba alioingia nao fainali.
  Baada ya kuhamishwa kutoka nafasi ya ulinzi wa kati hadi kuwa mshambuliaji, mchezaji kiraka wa KMC Sadallah Lipangile amefunga jumla ya magoli matano katika mechi tatu.
  Kati ya magoli hayo matano, manne amefunga katika michezo miwili ya mwezi Januari dhidi ya Singida United (05/01/2020) na dhidi ya Mtibwa Sugar (17/01/2020) huku bao la tano akilifunga wikendi iliyopita dhidi ya Azam FC (08/02/2020). 
  Katika orodha ya wafungaji bora kwenye ligi kuu, hadi sasa Sadallah anakamata nafasi ya 12 akiwa sawa na Ayoub Lyanga (Coastal), Bigirimana Blaise (Namungo), Hassan Dilunga (Simba), Innocent Edwin (Biashara), Shaban Hamis (Coastal) na Kelvin Kongwe (Kagera). Haya hapa magoli matatu kati ya matano aliyofunga.
  Aidha, Aristica Cioaba wa Azam FC ameibuka Kocha Bora wa mwezi huo akiwashinda Sven Vandenbroeck wa Simba na Malale Hamsini wa Polisi Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CIOABA AWAPIKU VANDENBROECK NA MALALE HAMSINI TUZO YA KOCHA BORA LIGI JUU JANUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top