• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 22, 2020

  AZAM FC YATOZWA FAINI SH MILION 1 KWA KUCHELEWA KUTOKA UWANJANI MECHI NA COASTAL

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imetozwa faini ya Sh 1,000,000 kwa kosa la timu hiyo kuchelewa kutoka uwanjani kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union FC Februari 15, mwaka huu Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 
  Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Februari 21, 2020 ilipitia taarifa mbalimbali za mechi ya Ligi Kuu Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) zinazoendelea hivi sasa.
  Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almasi Jumapili Kasongo kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba hata Kamishna alipowaita Azam FC walikaidi amri ya kutoka vyumbani na kipa wa timu hiyo alichelewa zaidi na alipofika uwanjani alishindwa kuwapa mikono wachezaji wa Coastal Union walioshinda 2-1.
  Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(43) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichofanyika jana kupitia taarifa mbalimbali za mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili (SDL) zinazoendelea hivi sasa nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YATOZWA FAINI SH MILION 1 KWA KUCHELEWA KUTOKA UWANJANI MECHI NA COASTAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top