• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 13, 2020

  AGRREY MORRIS APIGWA FAINI YA KWA KUGOMA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Azam FC, Agrrey Moris amepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.200,000/=(Laki Mbili) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
  Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
  Nayo klabu ya Polisi Tanzania imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.1,500,000/=(Milioni Moja na Laki Tano) kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi wa kuingia Uwanjani katika mechi iliyochezwa Februari 04,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

  Kamati imesema adhabu hiyo pia imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AGRREY MORRIS APIGWA FAINI YA KWA KUGOMA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top