• HABARI MPYA

    Sunday, July 05, 2015

    RAIS WA TFF AHUDHURIA KONGAMANO CANADA

    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na katibu mkuu wa TWFA Amina Karuma (kulia)

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anashiriki katika kongamano la Fainali za Dunia kwa Wanawake zinazofanyika Vancouver- Canada kwa siku tatu kuanzia tarehe 3 - 5 Julai mwaka huu.
    Katika kongamano hilo Malinzi ameambatana na katibu mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma.
    Kongamano hilo la soka la Wanawake linahudhuriwa na nchi 209 wanachama wa FIFA, ambapo hufanyika kila baada ya miaka minne, pindi zinapofanyika fainali za Dunia kwa wanawake.
    Miongoni mwa wachangiaji wa kongamano hilo ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya FIFA, ambaye pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha soka cha nchini Burundi, Lydia Nskera.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS WA TFF AHUDHURIA KONGAMANO CANADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top