• HABARI MPYA

    Friday, July 03, 2015

    RAIS MUSEVENI KUIONGOZA UGANDA KESHO DHIDI YA STARS NAKIVUBO, MBONA KAZI IPO!

    Na Baraka Kizuguto, KAMPALA
    RAIS wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni atahudhuria mchezo wan chi yake dhidi ya Tanzania, Taifa Stars kesho Saa 10:00 jioni Uwanja wa Nakivubo, Kampala.
    Mecho hiyo ya kesho ni mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2016 Rwanda na mgeni rasmi atakua Rais Museveni.
    Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Boniface Mkwasa, kiliwasili jijini Kampala jana usiku na kimefikia katika hoteli ya Grand Global iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.
    Taifa Stars imefanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Nakivubo yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe utakaofanyika kesho jioni.
    Rais Museveni (kushoto) akipiga danadana mbele ya wachezaji wa The Cranes miaka miwili iliyopita. Kesho atakuwapo uwanjani vijana wake wakimenyana na Taifa Stars
    Wachezaji wa Taifa Stars wakifanya mazoezi leo mjini Kampala

    Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema, anashukuru vijana wake wamefika salama wote, hali nzao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu, kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo kesho watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
    Akiongelea hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa amesema hali ya hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na Tanzania, mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo tayari. 
    Wakati huo huo mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam kuungana na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu ya Tanzania itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.
    Taifa Stars inatakiwa kushinda maba4-0 ili kusonga mbele, baada ya awali kufungwa mabao 3-0 Zanzibar wiki mbili zilizopita. Baada ya kipigo hicho, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimfukuza kocha Mholanzi, Mart Nooij na wasaidizi wake wote na kumteua Mkwasa, ambaye anasaidiwa na Hemed Morocco, kocha wa makipa Manyika Peter chini ya Mshauri wa Ufundi, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden'.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS MUSEVENI KUIONGOZA UGANDA KESHO DHIDI YA STARS NAKIVUBO, MBONA KAZI IPO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top