• HABARI MPYA

    Tuesday, July 16, 2013

    YANGA KUCHEZA NA TIMU MPYA YA LIGI KUU NIGERIA KESHOKUTWA TAIFA

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 7:25 MCHANA
    MABINGWA wa Bara, Yanga SC wanatarajiwa kucheza na Three Pillars ya Nigeria KESHOKUTWA (Alhamisi) katika mchezo wa kirafiki kujianda na msimu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mratibu wa mechi hiyo, Salum Mkemi ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba, timu hiyo kutoka Jiji la Lagos iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao, ipo nchini kwa takriban siku 10 kwa zaira ya mafunzo.
    Atacheza? Mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Ogbu Brendan aliyewasili jana huenda akaichezea kwa mara ya kwanza timu yake hiyo mpya keshokutwa

    Amesema timu hiyo imekuja na wachezaji 17 tu na makocha wao wawili na imefikia katika hoteli ya Itumbi, Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam na muda wote huo imekuwa ikijifua vikali.
    Mkemi, amesema mbali na kucheza na Yanga, wapo katika mazungumzo ili timu hiyo icheze pia na Simba SC, Coastal Union ya Tanga, Azam FC na Mbeya City ya Mbeya.
    Amesema kama watafanikiwa kupata michezo hiyo kabla ya Julai 30 wanaweza wakaongeza ratiba ya mechi. “Hii timu inatakiwa kuondoka Julai 30 hapa nchini, sasa kama itatokea timu iliyo tayari kucheza nayo ndani ya muda huo, tutaipa nafasi,”alisema Mkemi.  
    Hadi sasa, Yanga SC imekwishacheza mechi tatu za kujiandaa na msimu mpya na kufungwa moja na kutoka sare mbili. Ilitoka sare ya 1-1 na Express ya Uganda mjini Mwanza kabla ya kufungwa na timu hiyo katika mchezo wa marudio Shinyanga na baadaye kutoka 0-0 na Rhino FC mjini Tabora, ambayo imepanda Ligi Kuu pia msimu ujao.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA KUCHEZA NA TIMU MPYA YA LIGI KUU NIGERIA KESHOKUTWA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top