• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 28, 2013

  BALE AKASIRIKA ILE MBAYA SPURS KUKATAA OFA YA PAUNI MILIONI 82 KUMUUZA REAL MADIRD...NA HANA HAMU TENA NA JEZI ZAO NYEUPE

  IMEWEKWA JULAI 28, 2013 SAA 6:40 MCHANA
  NYOTA wa Tottenham, Gareth Bale amekasirika baada ya klabu kupiga chini ofa ya kuvunja rekodi ya dunia ya usajili kwa ajili yake Pauni Milioni 82 kutoka Real Madrid.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hakuwepo kwenye mechi ya kujiandaa na msimu ya klabu yake mjini Hong Kong jana- na hajisikii kuendelea kuvaa jezi nyeup za Tottenham tena.
  Kocha Andre Villas Boas aliamua kutomjumiisha nyota huyo wa Wales katika michuano ya wiki hii Barclays Asia Trophy kutokana na matatizo ya misuli. Lakini ukweli ni kwamba, mchezaji huyo yuko fiti kucheza- lakini wamemvuruga.
  Bale out: Will Welsh wizard been seen again in Tottenham shirt?
  Bale nje: Mchezaji huyo wa Wales ataonekana tena kwenye jezi nyeupe za Tottenham shirt?
  Alielekeza moyo wake kwenda Madrid kucheza Ligi ya Mabingwa sambamba na nyota wa soka akina Cristiano Ronaldo, Mesut Ozil, Luka Modric na Karim Benzema.
  Lakini uamuzi wa mwisho juu ya ndoto zake za kuondoka upo kwa Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, ambaye amekuwa akihakikisha Bale anamalizia Mkataba wake wa miaka mitatu.
  Na kutokana na Wales kukosa nafasi ya kufuzu katika Fainali zijazo za Kombe la Dunia, Bale anaona ni vyema ajakaribu bahati yake katika michuano mikubwa Ulaya na akiwa anaelekea kutimiza miaka 25, katika kipindi chote alichocheza soka, amecheza hatua hiyo ya michuano mara moja tu.
  Prospect: Danny Rose was particularly impressive for Spurs in the 6-0 win
  Alikosekana: Bale alikosekana kikosini Spurs ikiua 6-0 dhidi ya China Kusini Jumamosi
  Ikicheza bila Bale, Spurs iliifunga China Kusini mabao 6-0 katika mechi iliyochezwa kwenye mvua Hong Kong. Mechi ijayo ya kirafiki ya Tottenham ni dhidi ya Monaco Jumamosi na Villas Boas amesema: "Kuna uwezekano mkubwa yeye (Bale) atakuwa fiti. Atakuwa fiti kujiunga na timu kwa mazoezi Jumatano,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BALE AKASIRIKA ILE MBAYA SPURS KUKATAA OFA YA PAUNI MILIONI 82 KUMUUZA REAL MADIRD...NA HANA HAMU TENA NA JEZI ZAO NYEUPE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top