• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 21, 2013

  YANGA ILIVYOKATAA KUFANYWA KAMA SIMBA SC NA URA UWANJA WA TAIFA LEO

  IMEWEKWA JULAI 21, 2013 SAA 2:55 USIKUMfungaji wa bao la pili la Yanga SC, katika sare ya 2-2 na URA ya Uganda katika mchezo wa kirafiki, jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jerry Tegete akipongezwa na wenzake baada ya bao hilo la kusawazisha.

  Umetukomboa; Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Tegete

  Mfungaji wa bao la kwanza la Yanga SC, Didier Kavumbangu kulia akipongezana na wenzake

  Messi wa Jangwani; Abdallah Mnguli wa Yanga akiwatoka mabeki wa URA

  Jerry Tegete akiwatoka mabeki wa URA

  Mnisamahe; Jerry Tegete akionyesha ishara ya kuomba msamaha mashabiki ambao wamekuwa wakimzomea anapokosa mabao, baada ya kufunga bao muhimu leo

  Said Bahanuzi alicheza winga ya kulia na alipiga krosi nzuri kadhaa

  Said Bahanuzi pia alikuwa mwiba leo

  Mpira uende, wewe ubaki; Beki Juma Abdul akimdhibiti Derick Walullya wa URA

  Didier Kavumbangu akimkimbiza Derrick Walullya 

  Kavumbangu akimruka kipa wa URA, Yassin Mugabi aliyefanikiwa kuokoa mpira miguuni mwa mshambuliaji huyo wa Yanga SC

  Kocha Mholanzi wa Yanga SC, Ernie Brandts kulia, akiwa na Wasaidizi wake Freddy Felix Minziro, Razack Ssiwa na Daktari Nassor Matuzya

  Walipofufuka; Mashabiki wa Yanga kwa muda mrefu walikuwa wamemwagiwa maji, kabla ya kuzinduka dakika za lala salama kwa mabao ya Kavumbangu na Tegete 

  Huyu hatari; Lutambi Yayo akishangilia bao la pili aliloifungia URA leo. Mchezaji huyo alifunga mabao yote dhidi ya SImba SC jana na leo pia kafunga yote. 

  Kikosi cha URA leo

  Kikosi cha Yanga SC leo

  Shabiki wa Yanga SC, wakati timu yake ipo nyuma kwa mabao 2-0

  Gwiji akiombeleza; Kipa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Kitwana Manara 'Popat' kulia akiwa amesimama kuomboleza kifo cha kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mjerumani Bert Trautamann aliyefariki dunia juzi nyumbani kwake nchini Hispania.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA ILIVYOKATAA KUFANYWA KAMA SIMBA SC NA URA UWANJA WA TAIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top