• HABARI MPYA

    Saturday, July 27, 2013

    SIMBA NA YANGA PEKEE ZIMESHINDWA KUMPA HESHIMA HII RAIS KIKWETE HADI ANAKARIBIA KUONDOKA IKULU

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala, IMEWEKWA JULAI 27, 2013 SAA 6:00 MCHANA
    NANI asiyejua rais Jakaya Mrisho Kikwete ni mwanamichezo mzuri- akianzia kwenye kucheza mpira wa kikapu, soka kidogo shuleni na baadaye kuwa mpenzi mkubwa wa michezo.
    Na inafahamika Rais Kikwete ni mpenzi na mwanachama wa Yanga SC, moja ya klabu kongwe Tanzania.
    Tangu ameingia Ikulu mwaka 2005, akimpokea Benjamin Mkapa, Rais Kikwete amefanya mengi kwa ajili ya michezo kwa ujumla Tanzania na zaidi amekwamishwa na uongozi mbovu katika sekta hiyo.
    Jezi ya Brazil; Rais Luiz Lula Da Silva wa Brazil akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi namba 9 ya Brazil alipotembelea nchini humo

    Rais Kikwete amejaribu na haijalishi ndoto zake hazijatimia kwa kuangushwa na viongozi wabovu, walioweka mbele maslahi binafsi na wanaovamia sekta hiyo pasi na ufahamu nayo.
    Katika soka, huko ndiyo JK kafanya mengi- tulikwishasahau habari za makocha wa kigeni, lakini chini ya JK tumesahau habari za makocha wa klabu kuazimwa wafundishe timu za taifa.
    Mkurugenzi wa Azam FC, Abubakar Bakhresa akimkabidhi jezi Rais Kikwete



    Marcio Maximo akimpa Rais Kikwete zawadi ya jezi ya timu yake anayoifundisha ya Democrata nchini Brazi

    Meya Adam Kimbisa akimpa Rais Kikwete jez ya Ronaldo Real Madrid
    Timu nyingi, wachezaji kadhaa na hata viongozi wa mataifa mbalimbali wameonyesha kutambua upenzi wa Rais JK katika michezo kwa kumpa jezi wakati tofauti.
    Nchini Tanzania, ni klabu ya Azam FC pekee iliyompa Rais JK jezi, wakati katika kabati lake ana jezi ya Real Madrid na Barcelona za Hispania, Sunderland na Newcastle za England.
    Mchezaji Nizar Khalfan wakati anacheza Vancouver Whitecaps ya Canada naye alimpelekea jezi ya heshima Rais JK. 

    Dwight Howard wa Orlando Magic, akimkabidhi Rais Kikwete zawadi ya jezi Ikulu Dar es Salaam 

    Rais Kikwete naye alimzawadia Didier Drogba jezi ya Taifa Stars

    Nizar Khalfan akimpa Rais Kikwete jezi ya Vancouver Whitecaps wakati anacheza Canada. Kwa sasa Nizar amerudi nyumbani na anachezea Yanga SC
    Wakati akiwa amebakiza miaka miwili kabla hajaondoka Ikulu ya Dar es Salaam, iliyo pembezoni mwa Bahari ya Hindi, ajabu Rais JK hana jezi ya Simba wala Yanga, klabu kongwe na za kihistoria nchini.
    Yanga wanapenda kutamba kwamba mmoja wa wanachama wao ni Rais JK, lakini wameshindwa kumpa heshima ya jezi tu na akiwa Ikulu, klabu imepitia katika tawala nne sasa, kuanzia Francis Kifukwe, Imani Madega, Lloyd Nchunga na sasa Yussuf Manji na wote hawakuona umuhimu huo.

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4 2012

    Rais Kikwete akipokea jezi kutoka kwa mmiliki na Mwenyekiti wa Sunderland, Ellis Short, Ikulu, Dar es Salaam
    Rais JK japokuwa anasemwa ni mpenzi wa upande wa pili, lakini jitihada zake kuisaidia Simba SC kuingia ushirika na Sunderland ya England zimeonekana wazi- ajabu Wana Msimbazi nao hawajaona umuhimu wa kumpa Rais JK heshima ya jezi.
    Kuna mambo madogo madogo tu ambayo ukiyafanya, ondoa fikra za kujipendekeza wazi yanakuweka katika mazingira fulani- Simba na Yanga wanapaswa kutambua hilo.

    Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushila Thomas akipokea jezi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Barceloma, kwa ajili Rais Kikwete

    Rais Kikwete akikabidhiwa jezi ya Seattle Sounders ya Marekani

    Rais Kikwete akipokea jezi ya New York Knicks toka kwa Rais wa TBF Mussa Mziya na Makamu wake Phares Magessa
    Sasa leo Barcelona wanamtumia jezi Rais Kikwete Dar es Salaam kutoka Katalunya, wakati timu za Kariakoo tu hapo zimeshindwa kumpelekea. Ikoje hii.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA PEKEE ZIMESHINDWA KUMPA HESHIMA HII RAIS KIKWETE HADI ANAKARIBIA KUONDOKA IKULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top