• HABARI MPYA

    Friday, July 19, 2013

    MAN CITY YAENDELEA KUPOKEA VIPONDO AFRIKA, YAPIGWA 2-1 NA AMAZULU LEO

    IMEWEKWA JULAI 19, 2013 SAA 6:00 USIKU
    BILA kocha hakuna ushindi hapa Afrika Kusini, Manchester City imemaliza mzunguko wa kwanza wa ziara yake ya kujiandaa na msimu kwa maumivu mjini Durban.
    Kuondoka ghafa kwa kocha Manuel Pellegrini na kutowasili kwa Alvaro Negredo na Stevan Jovetic kumeifanya City ifungwe kwenye Uwanja wa Moses Mabidha kwa bao la dakika za lala salama la penalti.
    Kilikuwa kipigo cha pili baada ya Jumapili kuchapwa mabao 2-0 na SuperSport mjini Pretoria, kocha Pellegrini akiukosa mchezo huo baada ya kusafiri ghafla kurejea nyumbani kwao Chile kwa sababu za kifamilia.
    Opener: Bongani Ndulula of AmaZulu scores the opening goal in their 2-1 defeat of Manchester City
    La kwanza: Bongani Ndulula wa AmaZulu akifunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City

    Kocha huyo mpya alipanga kikosi cha kucheza mechi hiyo kabla ya kuondoka kwenda Santiago, akimuanzisha mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30, Fernandinho sambamba na Yaya Toure katika safu ya kiungo kwa mara ya kwanza. 
    Wachezaji wa Pellegrini bado wanachanganya taratibu baada ya kurejea mazoezini kiasi kama cha wiki mbili kutoka mapumzikoni na David Silva na mchezaji mpya, Jesus Navas – ambaye ataungana na Negredo na Jovetic hawajaripoti.
    Equaliser: James Milner levelled for Manchester City
    La kusawazisha: James Milner aliisawazishia Manchester City
    Exit: Manuel Pellegrini flew home to Chile for personal reasons
    Ameondoka: Manuel Pellegrini amerejea nyumbani Chile kwa matatizo binafsi

    Mabao ya Amazulu yalifungwa na Ndulula dakika ya 20 na Van Heerden kwa penalti dakika ya 87, wakati la City lilifungwa na Milner dakika ya 26.
    Kikosi cha Amazulu kilikuwa: Kapini; Macala, Teyise, Msekeli, Hlanti; Madondo, Madubanya, Manqana, Zondi, Dlamini; Ndulula. 
    Man City: Hart/Pantilimon dk63, Richards/Zabaleta dk46, Kompany/Garcia dk46, Nastasic/Lescott dk69, Kolarov/Boyata dk75, Milner/Razak dk75, Toure/Rodwell dk46, Fernandinho/Barry dk69, Sinclair, Dzeko/Nimely dk75 na Nasri/Suarez dk69. Support: South Africans show their support for City
    Mashabiki: Mashabiki wa Afrika Kusini wakiisapoti Man City
    Temas
    In control: City captain Vincent Kompany takes a touch
    Nahodha wa City, Vincent Kompany akimiliki mpira
    Advancing: Edin Dzeko tries to break down a tough AmaZulu defence
    Edin Dzeko akijaribu kupasua ukuta wa Amazulu
    Getting forward: Samir Nasri dribbles past the opposition
    Samir Nasri akiambaa na mpira
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAN CITY YAENDELEA KUPOKEA VIPONDO AFRIKA, YAPIGWA 2-1 NA AMAZULU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top