• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 24, 2013

  ROONEY KUICHAGUA ARSENAL IWAPO ITATOKEA MIZINGUO YA KUMZUIA KUFANYA KAZI NA MOURINHO CHELSEA

  IMEWEKWA JULAI 24, 2013 SAA 6:00 MCHANA
  MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ataamua kwenda Arsenal iwapo tu ndoto zake za kufanya kazi na Jose Mourinho Chelsea litabuma.
  Manchester United imekataa kumuuza Rooney kwa wapinzani wake wakuu kwenye mbio za ubingwa, lakini mshambuliaji huyo bado anataka kuondoka Old Trafford.
  Pamoja na kwamba Chelsea ni chaguo la kwanza, mshambuliaji huyo wa England atakwenda Arsenal iwapo David Moyes na bodi ya United itakaata ofa nyingine ya Mourinho.
  Departing? Wayne Rooney is a target for both Arsenal and Chelsea
  Anaondoka? Wayne Rooney anatakiwa na Arsenal na Chelsea
  Arsenal ilitia mkono kwa Rooney, ambaye atatimiza miaka 28 mwaka huu, wakati alipowekwa benchi katika mazingira ya kutatanisha kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa nyumbani dhidi ya Real Madrid, Machi. 
  Arsenal imesema inaweza kulipa mshahara wa Rooney, anayelipwa Pauni 240,000 kwa wiki na amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake wa sasa. 
  Chelsea wanabaki kileleni katika ushindani wa ofa kubwa, wakiwa wametoa Pauni Milioni 23, jumlisha Pauni 2.5 zitakazoongezwa kwa vipengele.
  Baada ya kuumia nyama, Rooney alirejea kufanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa United, Carrington na ni matumaini klabu hizo mbili zitafikia makubaliano. Mkewe, Coleen anafurahia maisha ya London na mtoto wao kwa manufaa ya kazi yake.
  Jose Mourinho
  Arsene Wenger
  Ushindani: Jose Mourinho na Arsene Wenger wote wanapenda kumsaini Rooney kutoka United
  Ubora wa nyota huyo ndio unaomfanya Mourinho ajaribu kumhamishia Rooney Chelsea, lakini pia anamheshimu Arsene Wenger.
  Mshambuliaji huyo wa England, ambaye anaweza kuwa fiti kucheza wiki mbili zijazo, ameambiwa kocha wa Arsenal, Wenger atajenga timu yake kwa kumhusisha yeye.
  Hiyo inafuatia Rooney kusukumwa nje ya kikosi cha kwanza na Sir Alex Ferguson na hadhi yake kushuka chini ya kocha mpya, David Moyes.
  Under pressure? David Moyes could be on the verge of losing one of his best players
  David Moyes yuko kwenye hatari ya kupoteza moja ya nyota wake
  Rooney alifanya mawasiliano ya simu Moyes na Makamu Mwenyekiti, Ed Woodward baada ya kuibuka taarifa kwamba mshambuliaji huyo amekasirika kutokana na namna anavyochukuliwa katika klabu hiyo.
  Chelsea inajiandaa kuongeza ofa yake kwa ajili ya Rooney, lakini haitakuwa tayari kuzidisha Pauni Milioni 30. Ikiwa United itakataa kumuuza Chelsea- Arsenal watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kumpata.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ROONEY KUICHAGUA ARSENAL IWAPO ITATOKEA MIZINGUO YA KUMZUIA KUFANYA KAZI NA MOURINHO CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top