• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 25, 2013

  RATIBA LIGI KUU ENGLAND YABOMOLEWA, MECHI YA CHELSEA NA VILLA YARUDISHWA

  IMEWEKWA JULAI 25, 2013 SAA 4:51 USIKU
  MECHI ya Chelsea ya Ligi Kuu ya England nyumbani kwa Aston Villa imerudishwa nyuma kutokana na timu hiyo ya London kuwa mechi ya kuwania Super Cup ya UEFA, Ligi Kuu imethibitisha.
  Mabingwa wa Europa League, Chelsea walitarajiwa kumenyana na Villa Jumamosi Agosti 31, lakini sasa mechi hiyo itachezwa siku 10 kabla, Agosti 21 huku The Blues ikimenyana na Bayern Munich mjini Prague Ijumaa ya Agosti 30.
  Well played: Jose Mourinho will welcome the announcement Chelsea against Aston Villa has been moved
  Jose Mourinho mechi yake ya kwanza na Chelsea dhidi ya Aston Villa imerudishwa nyuma

  Mechi hiyo itamkutanisha kocha huyo wa zamani Real Madrid, Jose Mourinho na kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, ambaye kwa sasa anainoa Bayern na aliyetabiriwa kuwa chaguo la kwanza la Roman Abramovich kutua Chelsea kabla haijathibitishwa kutimkia kwake Munich.
  Mabadiliko hayo ya ratiba, yanamaanisha Chelsea, ambaye utafungua msimu Agosti 18 dhidi ya Hull, itacheza mechi mbili nyumbani ndani ya siku nne, kabla ya kusafiri kuifuata Manchester United, Agosti 26 ambako wakishinda watawaacha kwa pointi sita mabingwa hao wa Ligi Kuu.
  Rout: More good news for Chelsea fans as their side thumped an Indonesian All-Star team 8-1
  Habari njema kwa mashabiki wa Chelsea kuhusu Ratiba ya Ligi Kuu, baada ya ushindi wa 8-1 dhidi ya Indonesian All-Star
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RATIBA LIGI KUU ENGLAND YABOMOLEWA, MECHI YA CHELSEA NA VILLA YARUDISHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top