• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 21, 2013

  MAN UNITED WATINGA TENA CAMP NOU NA OFA NENE ZAIDI KWA AJILI YA FABREGAS, BARCA KUTOAMUA LOLOTE HADI KOCHA MPYA APATIKANE

  IMEWEKWA JULAI 21, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
  KLABU ya Manchester United imeijaribu tena Barcelona juu ya kumsajili kiungo Cesc Fabregas wakiweka ofa ya pili, Pauni Milioni 30, kiasi cha saa kadhaa baada ya David Moyes kufurahia ushindi wa kwanza akiwa kocha wa klabu. 
  Lakini mabingwa hao wa Ligi Kuu England, bado watalazimika kusubiri, kwani kwa sasa Barcelona wanasubiri uteuzi wa kocha mpya baada ya kujiuzulu kwa Tito Vilanova kutokana na matatizo ya kiafya. 
  United awali ilitoa ofa ya Pauni Milioni 26 wiki iliyopita kwa ajili ya Fabregas, Nahodha wa zamani wa Arsenal.
  Target: Cesc Fabregas is the subject of another Manchester United bid
  Mlengwa: Cesc Fabregas ameendelea kuwapeleka mbio Manchester United ambao sasa wameboresha ofa yaod
  Concern: Tito Vilanova has stepped down as Barcelona boss due to ill health
  Afya imemuengua: Tito Vilanova amejiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya

  Moyes anataka kusaini mchezaji mmoja wa nguvu tangu arithi mikoba ya Sir Alex Ferguson, lakini angalau jana alifurahia ushindi wa kwanza dhidi ya nyota wa Ligi Kuu ya Australia mjini Sydney, huku makinda Jesse Lingard na Danny Welbeck kila mmoja akifunga mabao mawili na Robin van Persie aliyetokea benchi akafunga la tano. 
  Timu hiyo sasa ikiwa inaelekea Japan kwa mechi nyingine mbili zaidi katika ziara yao ya dunia, Moyes atahamishia nguvu zake kwenye usajili, baada ya kushuhudia dau lake la Pauni Milioni 12 kwa Leighton Baines likikataliwa na kiungo wa Barca, Thiago akijiunga na Bayern Munich. 
  Eye on the prize: Manchester United boss David Moyes
  Kocha wa Manchester United, David Moyes

  Pamoja na hayo, kumekuwa na mazungumzo na Gareth Bale mwenye thamani ya Pauni Milioni 60, n a Mtendaji Mkuu, Ed Woodward akisema wana fedha za kumnunua yeyote wamtakaye, hivyo ni suala la klabu yake tu, Tottenham. 
  Kuondoka kwa Vilanova Nou Camp Ijumaa kumechanganya suala uhamisho wa Fabregas, ambaye jana alimfariji kocha wake huyo wa zamani kwenye Twitter, kwa kusema: "Ujaaliwe nguvu, Tito. Wote tupo pamoja nawe, nakuunga mkono,".' 
  Barca haitafanya uamuzi wowote juu ya wachezaji, hadi wapate kocha mpya.
  In form: Manchester United's Robin Van Persie and Danny Welbeck (right) celebrate after Welbeck's goals against the A-League all stars
  Wachezaji wa Manchester United, Robin Van Persie na Danny Welbeck (kulia) wakishangilia baada ya Welbeck kufunga bao dhidi ya A-League all stars

  Nyota wa zamani wa Barca, Luis Enrique anapewa nafasi kuvwa ya kupewa mikoba ya Vilanova, licha ya kwamba ni mwezi uliopita tu ametua Celta Vigo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED WATINGA TENA CAMP NOU NA OFA NENE ZAIDI KWA AJILI YA FABREGAS, BARCA KUTOAMUA LOLOTE HADI KOCHA MPYA APATIKANE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top