• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 21, 2013

  MNIGERIA WA YANGA 'AVUNJIKA' TAIFA KABLA YA MECHI NA KUONDOLEWA FIRTS ELEVEN HADI JUKWAANI

  Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 21, 2013 SAA 11:08 JIONI
  MSHAMBULIAJI Mniegria wa Yanga, Ogbu Brendan Chukwudi aliondolewa ghafla katika kikosi cha kwanza cha Yanga baada ya kuumia wakati akipasha misuli moto kujianda kuingia mchezoni dhidi ya URA ya Uganda, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
  Kocha Mholanzi, Ernie Brandts alimuondoa kabisa Chukwudi katika orodha ya wachezaji wanaoshiriki mechi ya leo na kumuanzisha Mrundi, Didier Kavumbangu, wakati Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye hakuwamo kwenye mpango wa leo, akavalishwa jezi na kuanza benchi. 
  Haruna Niyonzima wa pili kushoto ameanzia benchi. Mniegria kaumia wakati wa kupahsa na ameondolewa kabisa mechi ya leo. Wengine kulia Bakari Masoud na kushoto ni Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh na Abdallah Mguli.

  Mechi iko mapumziko hivi sasa na tayari URA wanaongoza bao 1-0, bao lililofungwa dakika ya 42 na Litumba Yayo, ambaye jana Watoza Kodi hao wa Uganda wakiilaza Simba SC 2-1, alifunga mabao yote. 
  Kikosi cha Yanga kilicgoanza sasa ni; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Salim Telela, Said Bahanuzi, Hamisi Thabit, Jerry Tegete, Didier Kavumbangu na Shaaban Kondo.
  Katika benchi wapo, Issa Kazembe, Bakari Masoud, Abdallah Mguli ‘Messi’, Notikel Masasi, Sospeter Maiga, Abraham Sembwana, Benson Michael, Issa Ngao na Haruna Niyonzima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MNIGERIA WA YANGA 'AVUNJIKA' TAIFA KABLA YA MECHI NA KUONDOLEWA FIRTS ELEVEN HADI JUKWAANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top