• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 26, 2013

  MAN UNITED CHUPUCHUPU KUFUNGWA NA LEO, ZAHA AINUSURU KULALA KWA BAO LA DAKIKA ZA LALA SALAMA

  IMEWEKWA JULAI 26, 2013 SAA 2:36 USIKU
  KOCHA David Moyes tayari amesema mwanzo wa Ligi Kuu ya England utakuwa mgumu, Manchester United, ikipambana na Chelsea na Liverpool ndani ya wiki mwishoni mwa mwezi ujao.
  Wazi hakutarajia mechi za ziara dhidi ya wapinzani Asia na Australia zitakuwa ngumu, ila habari ndiyo hiyo na leo imenusurika kulala mbele ya Cereo Osaka baada ya kulazimisha sare ya 2-2.
  Mechi za kujiandaa na msimu na kwa kujiweka fiti kwa ajili ya msimu, lakini leo bao la Wilfried Zaha limeinusuru United kupata kipigo cha tatu katika mechi nne katika ziara yake ndefu. 
  Wenyeji walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Sugimoto dakika ya 34, lakini Shinji Kagawa akasawazisha dakika ya 54, kabla ya wenyei kupata bao la pili dakika ya 63, lililofungwa na Minamino.
  Shukrani kwake, Zaha aliyeifungia United bao la kusawazisha akiwa ndani ya sita dakika ya 91. 
  Kikosi cha Man United leo kilikuwa: Lindegaard; Rafael/Fabio dk79, Smalling, Ferdinand, Buttner/Evra dk79, Young/Cleverley dk79, Giggs/Lingard dk79, Jones/Anderson dk46, Kagawa/Zaha dk58, Welbeck na Van Persie/Januzaj dk69.
  Cerezo Osaka: Jin Hyeon, Sakemoto, Fujimoto, Yama, Maruhashi, Yokoyama, Kusukami, Fabio, Sugimoto, Minamino na Edno.Last-gasp: Wilfried Zaha celebrates his last-minute equaliser for Manchester United (below)
  Wilfried Zaha akishangilia bao lake la dakika ya mwisho lililoinusuru Manchester United kuzama. Chini anafunga.
  Zaha scores United's equaliser
  Duel: United striker Danny Welbeck in action as David Moyes' men struggled to a 2-2 draw
  Danny Welbeck akipambana
  Pointing it out: Zaha's cameo rescued United a share of the spoils against Japanese side Osaka
  Zaha akishangilia Osaka
  Battle: Van Persie and Tatsuya Yamashita fight for the ball tussle for the ball
  Van Persie na Tatsuya Yamashita 
  Twisting and turning: Zaha in action during the match, flying down the wing for United
  Zaha akimuacha mtu chini
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED CHUPUCHUPU KUFUNGWA NA LEO, ZAHA AINUSURU KULALA KWA BAO LA DAKIKA ZA LALA SALAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top