• HABARI MPYA

    Sunday, July 28, 2013

    MAN PACQUIAO SASA ATAKA URAIS WA FILIPINO

    IMEWEKWA JULAI 28, 2013 SAA 9:03 ALASIRI
    BONDIA maarufu wa Filipino, Manny Pacquiao amesema kwamba anataka kugombea Urais wa nchi hiyos atakapotungika glavu zake.
    Mwanamasumbwi huyo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa kwenye siasa kwa miaka kadhaa sasa, tangu achaguliwe kwenye Bunge la nchi hiyo mwaka 2007.
    Akizungumza na AFP, Pacquiao amesema: "Wakati naanza ngumi, kwa sababu nilipanga, unajua nilifikiria kuwa bingwa. Hivyo wakati naingia kwenye siasa, ni kitu kile kile,".
    Heading for president? Filipino boxing hero and Sarangani congressman Manny Pacquiao
    Atakuwa Rais? Bondia wa Filipino na Mbunge wa Sarangani, Manny Pacquiao
    Back in the ring: Pacquiao's next fight is with America's Brandon Rios in November
    Anarudi ulingoni: Pambano lijalo la Pacquiao ni dhidi ya Mmarekani, Brandon Rios mwezi Novemba

    Pacquiao amekuwa bingwa wa dunia katika madaraja nane ya uzito tofauti, na kwa sasa ni Mbunge wa Sarangani nchini humo.
    Pambano lake lijalo atapigana na Brandon Rios wa Marekani, November 24 likiwa pambano la kwanza tangu apigwe na Juan Manuel Marquez, hilo likiwa pambano la tano kupoteza katika historia yake.
    Famous face: George Foreman was at the press conference with Pacquiao and Rios
    Sura maarufu: George Foreman alikuwepo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kutangaza pambano la Pacquiao na Rios

    Akizungumzia pambano lake lijalo na Rios, alisema: "Yuko sawa, lakini naweza kusema ni mpiganaji mzuri na anapenda kupigana kwa karibu, anapenda gumba kwa gumba(kidole).
    "Hili litakuwa pambano zuri-- matukio zaidi ulingoni. Ni matumani yangu hatakimbia,".
    working his way up: Pacquiao is currently a congressman in the Philippines for the district of Sarangani
    Pacquiao kwa sasa ni Mbunge Sarangani na anataka Urais
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAN PACQUIAO SASA ATAKA URAIS WA FILIPINO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top