• HABARI MPYA

    Sunday, July 28, 2013

    LIVERPOOL YAUA 3-0, SUAREZ...

    IMEWEKWA JULAI 28, 2013 SAA 12:05 JIONI
    MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameendelea kuitumikia Liverpool kwa shingo upande majira haya ya joto hata katika mchezo wa leo, ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Thailand, mjini Bangkok.
    Mshambuliaji huyo wa Uruguay, ambaye anataka kuondoka Anfield, aliingia Uwanja Rajamangala dakika 30 za mwisho.
    Suarez alikaribia kufunga baada ya kupewa pasi na Steven Gerrard, lakini akakosa.
    Mabao ya Liverpool leo yamefungwa na Coutinho dakika ya 17, Aspas dakika ya 49 na Gerrard dakika ya 60.
    Kikosi cha Liverpool leo kilikuwa: Mignolet, Enrique, Agger, Toure/Skrtel dk69, Johnson, Lucas, Allen/Alberto dk80, Gerrard, Coutinho/Henderson dk69, Aspas/Ibe dk63 na Borini/Suarez dk63.
    Thailand: Hathairattanakool, Butmathan, Sokam, Daosawang, Wannasri, Lasoh, Anan, Songkrasin, Kraisorn, Wongsa na Dangda.
    Hugs and smiles: Liverpool captain Steven Gerrard with two Thailand players after the friendly win
    Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard akiwa amewakumbatia wachezaji wawili wa Thailand baada ya mechi hiyo
    Opener: Philippe Coutinho celebrates his 1-0 goal against Thailand in the first-half
    La kwanza: Philippe Coutinho akishangilia bao la kwanza 
    Captain marvel: Gerrard salutes the crowd after scoring Liverpool's third
    Gerrard akiurushia busu umati, baada ya kufunga bao la tatu la Liverpool
    Ahead: Coutinho sweetly struck the goal past the diving Thailand defenders
    Coutinho akifunga kwa kuupitisha mpira katikati ya mabeki wa Thailand walioanguka
    Questions marks on his future: A disappointed looking Luis Suarez on the bench for Liverpool
    Hakieleweki: Luis Suarez akiinuka kwenye benchi
    Still going strong: Gerrard had a strong game in the middle of Liverpool's midfield
    anamaambaa
    Header: Suarez came on around the hour mark and hit the bar before the end of the game
    Suarez alipoingia alifanya vitu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIVERPOOL YAUA 3-0, SUAREZ... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top