• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 22, 2013

  ARSENAL YAENDELEA KUTISHA MASHARIKI YA MBALI, YAVUNA MVUA NYINGINE YA MABAO LEO JAPAN

  IMEWEKWA JULAI 22, 2013 SAA 1124 JIONI
  ANGALAU mambo yanakwenda kulingana na mipango uwanjani kwa Arsenal majira haya joto.
  Wakati klabu ikiendelea kusaka majina makubwa ya kusajili waliyoahidi mashabiki wao, malalamiko hayawezi kutkea katika mechi zao za kujiandaa na msimu.
  The Gunners imefunga bao lake la 17 katika mechi tatu za kujiandaa na msimu nchini Japan leo, kutokana na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya zamani ya Arsene Wenger, Nagoya Grampus.
  Olivier Giroud ameendeleza makali yake katika mwechi hizi za kujiandaa na msimu akitimiza mabao sita katika ziara ya Mashariki ya mbali, kabla mwanasoka wa kimataifa wa Japan, Ryo Miyaichi na Theo Walcott kufunga kitabu cha  mabao.
  Homecoming: Japanese starlet Ryo Miyaichi (right) is congratulated by Olivier Giroud (left) and Mikel Arteta (centre) after his first half penalty
  Nimekuja nyumbani: Winga wa Japan, Ryo Miyaichi (kulia) akipongezwa na wenzake Olivier Giroud (kushoto) na Mikel Arteta (katikati) baada ya penalti yake kipindi cha kwanza
  Ilikuwa ni hatua nyingine nzuri ya kujiejengea kujiamini kwa The Gunners katika ziara yao ya majira ya joto, vaada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Indonesian Dream Team na 7-1 dhidi ya Vietnam XI.
  Wenger, ambaye alijiunga na Gunners akitokea Nagoya Grampus mwaka 1996, alipata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wa Japan, ambao bado wanamkumbuka alipokuwa akifanya kazi na Nagoya, Dragan Stojkovic, mmoja wa wachezaji wake maarufu katika klabu hiyo.
  Na kocha huyo wa The Gunners alishuhudia timu yake ikimpa raha mapema tu baada ya Giroud kufunga bao zuri la kichwa dakika ya tatu akimtungua kipa Seigo Narazaki kufuatia krosi ya Tomas Rosicky kutoka kulia.
  Timu hiyo ya Ligi Kuu Englad ilitawala kipindi cha kwanza, Walcott, Ramsey na Miyaichi wote wakipoteza nafasi za kufunga kabla ya Gunners kufunga bao la pili dakika ya 26 baada ya Giroud kuchezewa faulo kwenye eneo la hatari.
  Mikel Arteta alikwenda kupiga mkwaju wa penalti, lakini akakosa na mpira ukamkuta Miyaichi, aliyeukwamisha nyavuni na kuifanya Gunners iende kupumzika ikiwa inaongoza 2-0.
  On fire: Giroud celebrates with Miyaichi (right) after opening the scoring - his sixth goal in three friendlies
  Goal getters: Giroud celebrates his sixth goal of the tour (left) while Miyaichi converts a sentimental penalty
  Moto bati: Giroud akishangilia na Miyaichi (kulia) baada ya kufunga bao la kwanza, likiwa kla sita katika mechi tatu
  Dominant: Bacary Sagna (left), used as an emergency centre-back in Laurent Koscielny's absence, wins a header
  Mtawala: Bacary Sagna (kushoto), ametumika kwa dharula katika beki ya kati kutokana na kukosekana kwa Laurent Koscielny
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL YAENDELEA KUTISHA MASHARIKI YA MBALI, YAVUNA MVUA NYINGINE YA MABAO LEO JAPAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top