• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 21, 2013

  NIYONZIMA AREJEA YANGA, MNIGERIA AMUWEKA BENCHI KAVUMBANGU LEO

  Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 21, 2013 SAA 9:38 ALASIRI
  HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amerejea leo kujiunga na klabu yake, Yanga SC baada ya mapumziko kufuatia kumalizika kwa msimu.
  Haruna ametua leo mchana na Ndege ya shirika la Rwanda, na amesema sababu ya kuchelewa kuja kujiunga na wenzake ni matatizo ya kifamilia.
  Amerudi; Haruna Niyonzima amerejea leo kuendelea na kazi Yanga SC

  “Unajua unapokuwa mbali na nyumbani kwa muda mrefu, mengi yanatokea huku nyuma hujui. Sasa unaporudi nyumbani lazima uhakikishe unafika kila sehemu, nashukuru tumemaliza salama na nimerudi kazini,”alisema Niyonzima alipozungumza na BIN ZUBEIRY mchana huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Haruna ameingia Uwanja wa Taifa na Yanga ambayo jioni hii inamenyana na URA ya Uganda katika mchezo wa kirafiki, lakini hayumo kabisa katika wachezaji wanaocheza. 
  Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Ernie Brandts amewaanzisha; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Salim Telela, Said Bahanuzi, Hamisi Thabit, Jerry Tegete, Brenden Mnigeria Ogbu na Shaaban Kondo.
  Katika benchi wapo, Issa Kazembe, Bakari Masoud, Abdallah Mguli ‘Messi’, Notikel Masasi, Sospeter Maiga, Abraham Sembwana, Benson Michael, Issa Ngao na Didier Kavumbangu. 
  Haruna Niyonzima amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili Yanga SC Mei mwaka huu baada ya kumaliza Mkataba wake wa awali wa miaka miwili.
  Kiungo huyo aliyetua Yanga SC mwaka 2011 akitokea APR ya Rwanda ambayo pia alihamia akitokea Rayon Sport ni miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango kwa Yanga msimu uliopita kutwaa mataji mawili, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na Ligi Kuu Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NIYONZIMA AREJEA YANGA, MNIGERIA AMUWEKA BENCHI KAVUMBANGU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top