• HABARI MPYA

    Tuesday, July 30, 2013

    MAJIGAMBO YA PELLEGRINI ANA SAFU BORA YA USHAMBULIAJI DUNIA NZIMA...SASA LINGANISHA NA SAFU ZA TIMU NYINGINE TOP FOUR, HALAFU...

    BAADA ya kumsajili Alvaro Negredo na Stevan Jovetic, kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ameanza kujitamba kwamba safu yake ya ushambuliaji ndiyo inatisha zaidi Ligi Kuu England.
    sambamba na Negredo na Jovetic, Pellegrini pia anaweza kuwatumia Sergio Aguero na Edin Dzeko, na hili linampa imani kocha huyo wa Man City kwamba wanne hao watatisha mabeki wa England na Ulaya kwa ujumla na kuipa timu hiyo taji la ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Alipoulizwa kama mastraika wa Man City ndiyo bora England, Pellegrini alisema; “Ndiyo nadhani hivyo, safu yangu ya ushambuliaji ni bora. Namfahamu vizuri Negredo kutoka La Liga, hivyo sishangazwi na jinsi anavyocheza.
    Hi there: New Manchester City arrivals Alvaro Negredo, Stevan Jovetic and Jesus Navas
    Hodi: Mastaa wapya wa Manchester City, Alvaro Negredo, Stevan Jovetic na Jesus Navas
    Alvaro Negredo at Manchester Airport
    Manuel Pellegrini at Manchester Airport
    Safarini: Pellegrini (chini ) na Negredo (juu) wakielekea Munich kutoka uwanja wa ndege wa Manchester Jumanne.Escalating: (left-right) Jack Rodwell, Gael Clichy and Javi Garcia at the airport
    Wanapanda: (Kushoto kwenda kulia) Jack Rodwell, Gael Clichy na Javi Garcia wakiwa uwanja wa ndege
    “Nadhani tunawashambuliaji wazuri pamoja na Dzeko. Wanaweza kucheza pamoja au akacheza Jovetic au Aguero. Tuna washambuliaji wanne wakali na hilo ndiyo unalihitaji kama unacheza Ligi Kuu na Ligi ya mabingwa kama timu ya ushindani.”
    Wakati majigambo ya Pellegrini yakionekana ni mapema mno, huku kukiwa na Robin van Persie na jeshi lake jirani yao jijini Manchester, takwimu zinathibitisha kwamba raia huyo wa Chile anakitu cha kujivunia.
    Kwa jinsi hali ya mambo ilivyo, City ndiyo timu pekee ya Ligi Kuu England inaingia msimu mpya ikiwa na washambuliaji wanne ambao wote walifunga mabao 10 na zaidi msimu uliopita.
    Negredo – ametua kwa pauni milioni 20.6 kutoka Sevilla – ndiyo alifunga mabao mengi zaidi kati ya washambuliaji waliopo City, alifunga mabao 25 kwenye La Liga msimu uliopita. 
    Pleased: Manuel Pellegrini is delighted with his striking set-up, now he has signed Negredo and Jovetic (right)
    Anaamani: Manuel Pellegrini anaamani baada ya kuwasajili Negredo na Jovetic (Kulia)
    Negredo ndiye mshambuliaji pekee wa City ambaye msimu uliopita alifunga mabao zaidi ya 20, Dzeko alipiga 14, Jovetic alifunga 13 (akiwa Serie A) na Aguero, 12. Jumla wote wanne msimu uliopita walifunga mabao 64 na kuwazidi kwa mabao safu ya ushambuliaji ya Man United.
    Kule Manchester United, washambuliaji ambao David Moyes inherits - Van Persie, Wayne Rooney, Danny Welbeck na Javier Hernandez – walifunga jumla ya mabao 49, huku RVP akitupia 26 mwenyewe na Welbeck akifunga bao moja tu.
    Safu ya ushambuliaji ya Moyes itaharibika zaidi kama Rooney ambaye alifunga mabao 12 msimu uliopita akiondoka na kutua Chelsea. 
    Japokuwa Rooney alifunga mabao machache kulinganisha na kiwango chake msimu uliopita, lakini alithibitisha kwamba ni hatari kutokana na kupiga pasi nyingi za mwisho (10) akiwafunika washambuliaji wote wa Ligi Kuu.
    Main man: Robin van Persie led the line for Manchester United last season
    Mwenyewe: Robin van Persie aliongoza mashambulizi ya Manchester United msimu uliopita
    Kule Stamford Bridge, kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye anawashambuliaji watatu tu kwenye kikosi chake cha wakubwa. Anapata auheni kutokana na kurudi kwa Romelu Lukaku aliyekuwa West Brom kwa mkopo, akifunga mabao 17 ya Ligi Kuu akiwa huko, anaungana na Demba Ba aliyecheka na nyavu mata 15 na Fernando Torres, aliyefunga mara nane tu kwenye ligi, msimu uliopita.
    Kwa ujumla wao safu ya ushambuliaji ya Chelsea ilifunga mabao 40 msimu uliopita, na wako nyuma sana kwa City na United na ndiyo maana Mourinho amepania kumsajili Rooney.
    Kule London Kaskazini hali ilikuwa tete na ndiyo maana Arsenal na Tottenham wote walishindwa kutoa upinzani kwenye ubingwa na ndio maana Andre Villas-Boas na Arsene Wenger wanahaha kwenye soko la usajili.
    Back in business: Romelu Lukaku impressed for West Brom and will stay at Chelsea this term
    Karudi kazini: Romelu Lukaku alifanya vizuri akiwa kwa mkopo West Brom na msimu huu atabaki Chelsea
    Washambuliaji watatu wa Tottenham Jermain Defoe, Emmanuel Adebayor na  Clint Dempsey – walifunga mabao 23 tu na hii inaeleza kwa nini Spurs walimtegemea sana Gareth Bale, ambaye anaweza kutua Real Madrid wiki chache zijazo.
    Kutokana na kukosa makali kwa safu yake ya ushambuliaji AVB anamtolea macho straika wa Valencia, Roberto Soldado. 
    Wenger kazi yake imekuwa ni kujaribu na kufeli kila anapotaka kumsajili mshambuliaji wa kiwango cha dunia wakati huu wa kiangazi, amepigwa za uso na Napoli kwa Gonzalo Higuain na sasa hivi anaonekana kugonga mwamba kwa Liverpool katika mbio zake za kutaka Luis Suarez.
    Bosi wa Arsenal amepania kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji ambayo ina Olivier Giroud, Lukas Podolski na Theo Walcott, ambao kwa pamoja walifunga mabao 36 msimu uliopita na walishindwa kuchuana na Manchester United waliowapa RVP. 
    Wakati straika ya Arsenal ikifunga nusu ya mabao ya City, ni wazi Wenger anakazi kubwa sana kuwafikia wapinzani wake. Na kwa kuangalia takwimu kitete hakipo kwa Wenger pekee.
    Olivier Giroud
    Emmanuel Adebayor
    Mastraika: Olivier Giroud wa Arsenal (Juu) na Emmanuel Adebayor wa Spurs (Chini)
    Takwimu safu za ushambuliaji timu zote msimu uliopita 
    Arsenal
    Chelsea
    MCFC
    Man United
    Tottenham
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAJIGAMBO YA PELLEGRINI ANA SAFU BORA YA USHAMBULIAJI DUNIA NZIMA...SASA LINGANISHA NA SAFU ZA TIMU NYINGINE TOP FOUR, HALAFU... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top