• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 20, 2013

  BARCELONA WAIKATA MAINI MAN UNITED, WAIAMBIA ISAHAU KABISA KUHUSU FABREGAS

  IMEWEKWA JULAI 20, 2013 SAA 6:45 MCHANA
  KLABU ya Barcelona imeiambia Manchester United isahau kumsaini Cesc Fabregas.
  Huku United wakiendelea kuibania Chelsea kwa Wayne Rooney, wanakutana na hali kama hiyo kwa Barcelona ambao wanasema hawawezi kumuuza nyota wao huyo.
  Ikiwa tayari imepiga chini ofa ya United ya Pauni Milioni 26 kwa ajili ya kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania, Makamu wa Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema: "Barca haitakaribisha ofa yoyote juu ya Cesc. Hahamishwi.’
  Optimist: David Moyes is hopeful over a transfer move for Cesc Fabregas
  Mbishi: David Moyes anatumai kumnasa Cesc Fabregas
  Top target: Manchester United are keen to capture Cesc Fabregas after missing out on Thiago to Bayern
  Mlengwa Mkuu: Manchester United inamtaka sana Cesc Fabregas baada ya kumkosa Thiago aliyetimkia Bayern
   
  United wanaendelea kukomaa na nia ya kumsajili Fabregas kwa sababu wanaamini anataka kuondoka Nou Camp.
  Wakati Mtendaji Mkuu, Ed Woodward alirejea Uingereza kushughulikia dili hilo, kocha Moyes aliweka wazi kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Sydney mapema leo.
  "Mtendaji Mkuu amekuwa akishughulikia suala hilo sasa na nipo kwenye mawasiliano naye. Natumai kufahamu zaidi siku ijayo. Nitapata taarifa zaidi juu ya mambo yanavyoendelea siku ijayo,"alisema.
  Pamoja na hayo, Arsene Wenger pia bado anajiamini kwamba Fabregas atarejea Emirates akiamua kuondoka Barcelona.
  Kiungo huyo amewaambia rafiki zake wa karibu London na Barcelona kwamba atarejea Ligi Kuu England tu kuchezea Arsenal, hali ambayo inavunja matumaini ya Moyes kumpata Mspanyola huyo. 
  Arsenal wanajua Fabregas atabakia kwa angalau miezi 12 mingine, lakini ikiwa kuna mabadiliko, The Gunners wapo nafasi ya mbele kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kwa Pauni Milioni 25.
  United inaendelea pia kumfukuzia Gareth Bale, winga wa Tottenham ambaye pia anatakiwa na Real Madrid. Moyes pia ni shabiki wa mchezaji wa Real, Luka Modric. Anahitaji viungo kuimarisha timu yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BARCELONA WAIKATA MAINI MAN UNITED, WAIAMBIA ISAHAU KABISA KUHUSU FABREGAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top