• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 27, 2013

  KIFO CHA STARS NAMBOOLE LEO, STARS ILIVYO...

  IMEWEKWA JULAI 27, 2013 SAA 3:09 USIKU
  Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Haroun Chanongo akimtoka beki wa Uganda katika mchezo wa leo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za michuano ya Ubingwa wa Mataifa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee dhidi ya wenyeji, Uganda, The Cranes kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda. The Cranes ilishinda 3-1 na kufanya ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 1-0 wiki mbili zilizopita mjini Dar es Salaam, hivyo imefuzu kucheza CHAN mwakani Afrika Kusini. 

  Simon Msuva akimtoka Habib Kavuma

  Mrisho Ngassa (kulia) na Athumani Iddi 'Chuji' wakigombea mpira na Nahodha wa Uganda, Hassan Waswa

  Nicolas Wadada wa Uganda, akimdhibiti Mrisho Ngassa 

  Amri Kiemba akipambana na wachezaji wa Uganda

  John Bocco akipiga kichwa katikati ya msitu wa wachezaji wa Uganda

  Kevin Yondan akiondosha mpira hatarini kwa kichwa dhidi ya mchezaji wa Uganda

  Ngassa na Wadada

  Salum Abubakar 'Sure Boy' akipiga shuti katikati ya wachezaji wa Uganda

  Chuji kulia na Said Kyevune wa Uganda kushoto

  Chuji akiondosha mpira kwenye hatari dhidi ya Habib Kavuma

  Frank Kalanda akimdhibiti Mrisho Ngassa

  Frank Domayo alilazimika kumsaidia sana David Luhende leo kabla ya kuumia na kutoka

  Mrisho Ngassa akiwania mpira dhidi ya wachezaji wawili wa Uganda

  Amri Kiermba akitia krosi pembeni ya Wadada

  Frank Domayo akimtoka Said Kyevune

  Domayo na Kyevune

  Sure Boy akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Uganda

  Domayo akipiga shuti

  Krosi ya Erasto Nyoni ikipitiliza, Ngassa hakuweza kunasa

  Kizaazaa langoni mwa Uganda

  Kocha wa Uganda, Milutin Sredojevic 'Micho' akimpongeza Brian Majwega kwa kazi nzuri

  Chuji anaosha...

  Kipa wa Uganda, Hassan Muwonge akidaka mpira dhidi ya Mrisho Ngassa kufuatia krosi ya Nyoni

  Muwonge akidaka kiulaini...ufupi ni tatizo wakati mwingine

  11 wa Uganda walioanza leo

  11 wa Stars walioanza leo

  Wajumbe wa Kamati ya Stars, Mh Zitto Zuberi Kabwe (kulia) na Jamal Rwambow wakati wimbo wa taifa wa Tanzania ukichezwa

  Mfungaji wa mabao mawili ya Uganda leo, Frank Kalanda akimfunga tela David Luhende

  Luhende akimdhibiti Majwega

  Wasswa akimpa paja Ngassa...hii aliigundua Gianfranco Zola mwaka 2009 Mrisho alipokuwa West Ham kwa majaribio, akamuambia akaongeze lishe

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KIFO CHA STARS NAMBOOLE LEO, STARS ILIVYO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top